JACK WA CHUZ, NJEMBA WAZUA UTATA HOSPITALI

No Comments


MWIGIZAJI Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ mwishoni mwa wiki iliyopita alizua utata katika Hospitali ya Aghakani ya mkoani hapa baada ya kunaswa akiuguzwa na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashid Said.
MWIGIZAJI Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ akutwa na njemba aliyejulikana kwa jina la Rashid Said.
Baadhi ya watu waliofika kumtembelea Jack aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Typhoid, walihoji juu ya ukaribu wa Rashid ambaye ni kinyozi mjini hapa na staa huyo ndipo paparazi wetu alipowauliza wawili hao kwa nyakati tofauti, kila mmoja akatoa jibu lake.
“Huyu ni shemeji yangu kwa bwana angu ambaye baada ya kupata taarifa za mimi kulazwa alifika hapa toka mwanzo na kunihudumia,” alisema Jack huku Rashid akisema:
“Jack ni rafiki yangu na kwamba baada ya mimi kupata taarifa za kuugua kwake, nilikuja kumhudumia.”
Jack baada ya kulazwa kwa muda hospitalini hapo, aliruhusiwa na kurejea nyumbani kwake, Dar.
back to top