RAIS wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ amefunguka kuwa mwigizaji Husna Idd ‘Sajent’ hakustahili kuwa mkewe licha ya kwamba walizaa naye mtoto mmoja.
Akizungumza na Global TV Online hivi karibuni, Chaz Baba alisema Sajent ni mwanamke mzuri lakini hana vigezo vya kuolewa na yeye kwani wote ni maarufu.
“Nilikuwa nampenda sana Sajent ila nilishindwa kumuoa kutokana na umaarufu wake ambao ulimnyima sifa ya kuolewa na mimi maana wote ni mastaa ingekuwa shida huko mbeleni,” alisema Chaz Baba.