Hayo yakiwa ni makubaliano makubwa katika historia ya miaka 38 ya kampuni hiyo.
Hatua hiyo inaonekana kama jitihada ya kuiendeleza sifa ya Apple katika soko la kusikiliza muziki kwenye mtandao.
Hatua hiyo inaonekana kama jitihada ya kuiendeleza sifa ya Apple katika soko la kusikiliza muziki kwenye mtandao.
Pamoja na ununuzi huo, waanzilishi wa Beats Jimmy Lovine na msanii wa mziki mtindo wa kufoka Dkt. Dre watajiunga na kampuni hiyo ya kiteknolojia.
Beats ilianzishwa na mzalishaji wa muziki Jimmy Lovine na nyota wa mziki wa kufokafoka, Dr. Dre, na mitambo hiyo imejulikana kuwa bora zaidi hadi siku za hivi majuzi.
Beats ilianzisha huduma ya muziki unaolipiwa mapema mwaka huu.
Apple ina huduma ya iTunes ambayo ndio kubwa zaidi duniani inayohusiana na mziki, na ilianzisha kituo cha radio cha iTunes mwaka uliopita.
Hata hivyo, huduma ya mziki ya Beats ina wateja wapatao 110,000 pekee waliojisajili ikilinganishwa na Spotify ilio na watu milioni 10 waliojisajiliwa.
CHANZO NI BBC SWAHILI