
Kama ilivyo kwa tuzo zozote maarufu duniani, mara nyingi ma’MC wa show
hizo huwa wanapenda kumwaga maneno mengi sana ya utani, ila hii ni kali zaidi,
bila kujijua mwenyewe wakati akiwa anaendelea kutangaza, alitokea kuwaponda
watu maarufu duniani, akiwemo Kim Kardashian ambaye anajulikana kama ni
mwanamke mwenye umbo zuri zaidi, “I’ve seen beautiful women here with butts
that make kimkardashian‘s look like Miley Cyrus.(“nimekuja hapa nimeona
wanawake wenye maumbo mazuri, yanavyomfanya Kim Kardashian aonekane kama Myle Cyrus”) – alitamka wazi wazi MC wa tuzo hizo za MTV MAMA.

Watu wenye maumbo kama Wema Sepetu na wanawake wengi wa huko
nchini South Africa achilia mbali wageni waaalikwa kutoka nchi mbali mbali
za africa, kwa jinsi walivyo umbika kwa asili ya maumbo yao ya ki-africa,
yalimfanya hadi MC ambaye ndiye mchekeshaji muigizaji maarufu huko
hollywood maarufu kama Marlon Wayans, ashundwe kujizuia na kutamka
maneno kama hayo hadharani.