Ostadh Juma Namsoma akiwa katika pozi.
MWISHONI mwa wiki iliyopita, nilipata simu kutoka kwa mmoja wa wadau wa safu hii, akinitaka niangalie katika mitandao ya kijamii, nione kipande cha video kinachomuonyesha msanii mmoja akimpigia magoti promota wa muziki na kumuomba msamaha.
Baada ya kuperuzi mitandao kadhaa, nikakutana na picha ya msanii wa muda mrefu lakini anayegoma kutoka, Pancras Ndaki ‘PNC’ akimpigia magoti promota anayetajwa kwa jina la Ostaz Juma, bosi wa Kundi la Mtanashati, ambalo linawamiliki wasanii kadhaa.
Niliitazama na kuisikiliza. Awali, nilipatwa na hasira kali dhidi ya Ostaz, kwani kwa jinsi ilivyo, haikufanyi ushindwe kufikiria kuwa ni yeye ndiye alisimamia upigwaji wake na baadaye kuisambaza mitandaoni,

kwani imekaa kwa namna isiyovutia.
Lakini baada ya kuisikiliza na kujipa muda kidogo wa kutafakari, nikajikuta nikipatwa na faraja kubwa kwa nilichokiona, tofauti na watu wengine ambao wameonyesha kukerwa mno na kitendo hicho, walichokiita ni cha kidhalilishaji, dhidi ya msanii kufanywa na promota.
Dogo PNC anamuomba msamaha promota, akimtaka amsamehe yeye na wenzake. Video ina tatizo moja tu, sehemu ya kosa walilofanya hadi wanalazimika kuomba msamaha haionekani. Hisia zinaniambia ni masuala ya muziki, kwa sababu siku za nyuma, msanii huyo aliwahi kuripotiwa kulihama kundi hilo.

Nimefurahishwa na tukio hili kwa sababu angalau limeonyesha sura halisi ya wasanii wetu, tofauti na ambavyo wadau wao wengi hawafahamu.
Wasanii wetu wana vipaji vikubwa sana, lakini wanakosa kujitambua. Kutojitambua kwao kunatokana na sababu nyingi, zikiongozwa na kukimbia kwao shule. Ninaposema shule, simaanishi madarasa peke yake, bali hata uelewa nje ya vyumba vya kufundishiwa. Tunapokuwa shule, hatufundishwi mbinu za kukabiliana na matapeli, bali tunapewa mwanga unaoweza kutusaidia kumtambua tapeli.
Wasanii wetu wanaamini kabisa kuwa bila uwepo wa mameneja, hawawezi kutoka. Tatizo lao linaanzia hapa. Kwao, meneja ni mwenye fedha, mtangazaji wa redio au televisheni, kwa sababu atasababisha kazi zao kuchezwa. Mbaya zaidi kwa wasanii wetu meneja ndiye bosi na yeye ni mfanyakazi.

Hawajui kuwa wao ndiyo matajiri, ndiyo wenye kuajiri na kufukuza mameneja. Hawajui kuwa wamiliki wa Lebo wanawahitaji wao zaidi kuliko wao wanavyozihitaji lebo. Msanii anaweza kutengeneza mabilioni yake bila kuwa na lebo, lakini ni miujiza ya karne kwa lebo kutengeneza fedha ya muziki bila kuwa na wasanii.
Katika hali ya kawaida ya kibiashara, kinachofanyika ni win to win situation, yaani kila mmoja afaidike.
Msanii ana mtaji wa sauti na tungo (ingawa siyo lazima, wakati mwingine anaweza kutungiwa) na mmiliki wa lebo au meneja kwa tafsiri ya wasanii wetu, ana fedha za kuwezesha studio na promo. Baada ya hapo kila mmoja anapata kulingana na makubaliano.

Lakini kwetu ni tofauti. Kutokana na ujinga wao, wasanii wetu wanafanywa watumwa wakati wao ndiyo msingi mkubwa wa fedha za mabosi wao. Kutokana na uelewa wao finyu, wamewaruhusu hawa wezi kujadiliana na watu wanaowahitaji kwa ajili ya shoo. Wakishapatana bei, tuseme labda na tajiri flani, hawa wezi, kwa kigezo cha umeneja au ukuu wa lebo, wao ndiyo humpatia kiasi wakitakacho wao, ambacho mara zote huwa ni kidogo.
Ndiyo maana utaona wanaoitwa mameneja wana miradi mingi lakini chanzo cha miradi yao ni jasho la wasanii. Hawa tunawajua, wanavimba matumbo na wenye dharau kubwa.
Kama vijana wetu wangekuwa wanajitambua na wenye uelewa, wasingenyanyasika. Lakini kwa sababu wametukuta mbumbumbu, hata kama wana hela ya kubadilishia mboga tu, watajifanya kumiliki mamilioni.

Wamekuta wajinga wanatumia vipande vya dhahabu kuchezea bao, wao wamechongesha vitufe vya mbao na kuwaletea. Kwa ujinga wa wasanii wetu wanadhani ni matajiri sana, kumbe wametumia vizuri fursa ya umbumbumbu wao.
Njia rahisi ya kuwafanya watu hawa kuondoka katika ramani, ni kwa wasanii kujitambua, kwamba wao ni matajiri. Makubaliano yawe ya wao kunufaika na siyo kila siku wanaendelea kuwa chini ya mtu. Lebo nyingi za Kibongo zinaendeshwa na wabinafsi, ambao hawataki mtu ajielewe, ndiyo maana utaona msanii anayeonekana kujua haki zake, huambiwa anajifanya mjanja na hupigwa vita kila kona. Mifano ya wasanii wa aina hii mnayo, waigeni au endeleeni kuwapigia magoti!