Msanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes amesema kitendo cha bosi wa Mtanashati
Entertainment, Ostaz Juma kuchukulia poa msanii wake, PNC kumpigia magoti akimuomba msamaha kisha kurekodiwa video iliyosambaa mtandaoni kimemuuma sana kwani kimewadhalilisha wasanii wa Bongo.
Akipiga stori, Dully alisema: “Imeniuma sana na nimemdharau jamaa kwa sababu kaonyesha dharau kwa wasanii wote na si PNC pekee, mbona wadau wengine wamekuwa hawafanyi hivyo? Tumekuwa tukiwakosea na wanatusamehe yanaisha bila watu wengine kujua, hii siyo sawa.”