KUPOTEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

No Comments
Tatizo hili kwa kifupi linaitwa ISD.
Ni tatizo linalowapata wanawake na wanaume. Tatizo huanza taratibu kwa mtu kutojihisi kama anapatwa na hali hii. Tatizo linapozidi kukua mwanamke
huathirika zaidi na kupata hali iitwayo ‘frigidity; yaani mwili wake unakuwa na ganzi au baridi kabisa na kukosa msisimko na raha ya tendo. Mwanaume hupoteza kabisa uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
Jinsi tatizo linavyotokea Hali ya tatizo hutokea kutofautiana kwa mwanaume na mwanamke, mara nyingi tatizo huanza endapo hakuna maandalizi ya kutosha kabla ya tendo. Ni vema kuwepo na maandalizi ambayo yataamsha msisimko ambao pia utaamsha kemikali husika za mwili na kukufanya uweze kufurahia.
Mwanamke anayepatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa yupo katika hatari ya kupatwa na tatizo hili, mwanamke ambaye anaumwa na tumbo chini ya kitovu mara kwa mara, anayetokwa na damu kwa muda mrefu ukeni, na yule anayetokwa na uchafu ukeni kwa muda mrefu ni miongoni mwa wanaoathirika na tatizo hili baya ambalo huvuruga mahusiano. Tatizo huwapata pia wale ambao wapo katika migogoro ya kimapenzi, watumiaji wa madawa ya kulevya na wanawake wenye magonjwa sugu na wanaotumia dawa kwa muda mrefu, mfano wenye magonjwa ya kisukari, kansa, shinikizo la juu la damu, kifua kikuu na ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa na maambukizi ya HIV.
Wenye matatizo ukeni pia wapo katika kundi hili. Wanaume ambao hupoteza hamu ya tendo la ndoa aidha hupoteza nguvu za kiume, au hupungukiwa nguvu za kiume kwa kiasi kikubwa. Wanaume wanaokuwa katika kundi hili ni wale walevi ambao kila siku lazima wanywe pombe, wavutaji sigara sana, wanaotumia madawa ya kulevya, hasa bangi. Wengine ni wanaosumbuliwa na magonjwa sugu, lishe duni, mwili kukosa mazoezi na msongo wa mawazo pia huathiri msisimko kwa mwanaume.
Magonjwa ya zinaa, kisukari, kifua kikuu na shinikizo la juu la damu pamoja na unene uliopitiliza pia huchangia tatizo. Mwanaume huanza tatizo taratibu, kwanza huhisi kupoteza hisia za tendo na uume kushindwa kusimama wakati anapohitaji iwe hivyo, pili hujikuta anawahi kumaliza tendo kabla mwenzie hajawa tayari, tatu anaweza kupata uchovu mkali mara anapomaliza tendo na mwili wote kulegea na kushindwa kuendelea. Wengine huwa wagonjwa kabisa muda huo. Hali huendelea hadi mtu anapoteza kabisa hamu na hisia.
Uchunguzi 
Tatizo hili huchunguzwa hospitali. Hakuna dawa maalum ya kuongeza nguvu za kiume au kupata hisia za kiume au msisimko wa tendo hadi ufanyiwe uchunguzi wa kina kujua ni nini kinasababisha.
Uchunguzi hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya kwa madaktari wa masuala ya uzazi ambapo utapata ushauri na tiba.
Nini cha kufanya?
Epuka kutumia madawa bila ya uchunguzi wa kina hospitali, tumeona sababu nyingi za tatizo hili kwa mwanaume na mwanamke, sasa huenda wewe unayo moja au zaidi kati ya hizo, kutumia dawa bila kufahamu chanzo au kutibu chanzo ni kupoteza pesa, muda na dawa.
back to top