Mis Tanzania auza Jeep yake…huyu ni Salha israel aliyesimama sana katika ma-miss hapa Tzee kwani kuanzia rangi yake muonekano na hata kujiamini. Baada ya kuona mambo hayamuendei poa huku gari hiyo ikiwa mzigo mzito wa mafuta na huku anatakiwa kwenda mbio za maisha ya mjini na foleni zetu Miss huyo aliamua kulitia sokoni gari hilo na kutafuta gari inayoendana na maisha yake kwa sasa.
Miss TZ huyo amekua akionekana kwenye gari aina ya IST ambayo ni affordable kabisa kwani akiweka lita kumi tu anakwenda anapotaka hapa mjini bila ya kufungua dirisha. Huku akiwa hapatikani kujibu swali hilo lakini tulipowatafuta Ma-miss alioshiriki nae mwaka 2011 walisema huwa wanakutana nae sana mitaani na night club lakini hawamuoni na Jeep hiyo ila IST so hawaelewi Jeep iko wapi…
