Kukiwa bado kuna hali ya sintofahamu kati ya mapenzi ya Justin Bieber na Selena Gomez, hivi karibuni Justin alifanya kitendo ambacho kinazidi kuwaweka watu njia panda juu ya mahusiano yao. Hii ilitokea baada ya Justin Bieber kupost picha kwenye mtandao wa Instagram ya yeye akiwa amekumbatiwa kichwa na ex wake Selena huku kukiwa na caption isemayo “ur love is unconditional”, hii ilikuwa Jumatano ya tarehe 11/06/2014. Lakini cha kushangaza, post hiyo haikudumu, Justin alii delete muda mfupi tu baada ya kui post na kuacha watu wakiwa na maswali kibao, je alikuwa anamaanisha alichoki post? Kwanini amei delete? Ni maswali ambayo majibu yake nadhani watakuwa nayo wawili hao.
Hivi karibuni Bieber na Selena hawako kwenye good terms kuanzia kipindi flani hivi cha April, na hawajaonekana pamoja toka kipindi hicho.Kama kutakuwa na update yeyote ile, basi usitie shaka, pamojasisi.blogspot.com ipo ili ikupe mchongo kamili in next few days..
