KARIBUNI katika Let’s Talk About Love. Bila shaka mu wazima wa afya. Tunaendelea na mada yetu iliyoanza wiki iliyopita. Somo hili ni muhimu sana kwa wapendanao kujua ahadi ambazo zinaweza kuwa na nakshi katika mapenzi na zile ambazo huleta migogoro katika uhusiano.
Niliacha kwa kueleza machache wiki iliyopita. Ahadi zenyewe ni zipi na zinakuwaje? Tuendelee na somo letu?
UWEZO WA FAMILIA
Baadhi ya wanaume wanapokutana na wenzi wao kwa mara ya kwanza, ili wasidharaulike huanza kujisifu kwamba wanatoka katika familia zenye uwezo.
Baadhi ya wanaume wanapokutana na wenzi wao kwa mara ya kwanza, ili wasidharaulike huanza kujisifu kwamba wanatoka katika familia zenye uwezo.
Kwa kutumia njia hii, huwa na imani kwamba watakubaliwa kwa urahisi zaidi kwa vile wanatoka katika familia hizo. Hili ni tatizo katika siku za mwanzo wa uhusiano, kwanza kwa mwanamke mwenye akili, atakudharau badala ya kukupa heshima.
Atakuona mwanaume tegemezi ambaye unajisifu kwa sababu ya mali za familia. Hata hivyo, hii si sifa kubwa ambayo itamfanya mwanamke mwenye uelewa akukubali, kwa sababu unaonekana una majigambo.
Mwanaume thabiti hazungumzii juu ya familia yake. Mtu wa aina hii humuahidi mpenzi wake kumsaidia kwa kuwa anatoka katika familia yenye hali nzuri kifedha. Huu ni ushawishi wa kizamani sana.
Hata hivyo, utafiti unaonesha kwamba asilimia kubwa ya wanaume wanaotumia gia hii kupata wanawake, si kweli kwamba wanatoka katika familia za aina hiyo. Hutumia kama njia tu, lakini baadaye hubainika kwamba walikuwa hawana uwezo kama waliosema awali.
Athari inayoweza kupatikana kutokana ahadi hii ni pale ambapo unagundulika kuwa huna uwezo huo, lakini tayari mmeshazama kwenye penzi zaidi. Inawezekana awali wakati unaanzisha uhusiano naye, hukuwa katika kilele cha mapenzi sana.
Yawezekana ulimuona kama mwanamke wa kuzugia ndiyo maana ukatumia gia kubwa ili umpate, lakini baada ya kuwa naye kwa muda, ukagundua kuwa moyo wako umempenda zaidi ya ulivyokuwa ukifikiria.
Kinachotokea hapa ni kwamba, wakati ukiwa umeshaamua kumpenda na kuwa naye, anagundua kwamba yupo na mwanaume muongo. Hata kama alikuwa anakupenda kwa kiwango gani, hawezi kukubali kuendelea na mwanaume wa aina yako.
BOSI KAZINI
Wengine huwadanganya wenzi wao wanapokutana nao mara ya kwanza kuwa wana nafasi za juu katika sehemu zao za kazi yaani mabosi. Wanaamini kwa kutumia gia hiyo, itakuwa rahisi zaidi kumpata mwanamke huyo.

Hata kama ni kweli wewe ni mkuu wa idara unayofanyia kazi ofisini kwako, si hoja muhimu inayohitajika kwa mwanamke unapokutana naye mara ya kwanza.
Kwa mwenye uelewa atakudharau kwa kujikweza kwako, lakini mwingine anaweza kukubali si kwa sababu ya uongozi wako kazini, bali kwa mapenzi yake ya dhati kwako, lakini ndani ya moyo wake akiwa na malengo mengine.
labda unaweza kumuahidi kuwa kwa ubosi wake na namna unavyofahamiana na watu wengi, utaweza kumsaidia kupata kazi au kumwajiri kabisa. Tayari ameshakuwa na imani kuwa atapata kazi akiwa katika uhusiano na wewe.
Ataingia kwenye mapenzi akiwa anakupenda lakini mtazamo wake juu yako utakuwa mwingine. Kwamba atakuwa anaishi na bosi.
Ni kweli mapenzi si fedha, lakini inakuwaje pale unapomhakikishia mpenzi wako kuwa unazo, wakati anajua kuwa huna kitu?
Ni kweli mapenzi si fedha, lakini inakuwaje pale unapomhakikishia mpenzi wako kuwa unazo, wakati anajua kuwa huna kitu?
FIKIRI ZAIDI KUHUSU AHADI
Kikubwa rafiki zangu ninachotaka kuwaambia hapa ni vyema kupima kauli zenu kabla ya kumwambia mwenzako. usiahidi vitu ambavyo kamwe unajua kabisa huwezi kuvitimiza. Achana na mambo ya kizamani, mweleze mwenzako hali halisi ya maisha yako.

Kuwa huru, mapenzi si mali kama baadhi ya watu wanavyodhani. Kuwa wazi, naye atakuheshimu kutokana na ukweli wako. Kwa leo unaweza usione madhara ya kutoa ahadi hewa, lakini utakapokolea kwenye mapenzi, halafu ukashindwa kutimiza yale uliyokuwa unayaahidi ndiyo mwanzo wa
matatizo.
matatizo.