Haya niliyapata kutoka kwa mshauri wa masuala ya mahusiano, ndoa na vijana
Frederick Kyara. Hizi ni baadhi tu nakuwekea hapa japo kuna vitu pia wanawake
hawavipendi kutoka kwa wenzi wao wanaume. Nayo ni haya hapa, ungana nam
i kujadili jambo hili ambalo kwangu nimeona ni changamoto au niseme sikujua.
1. Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya na wenzi waoMwanamke
unapotaka mwanaume afanye jambo usimwambie alifanye bali fanya kama
una mpa ushauri. Kwamba John hivi kwa nini tusiweke balbu hapa kwenye
korido maana kuna giza kweli. Badala ya hivi wewe John huoni hapa kwenye
korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa hujabadilisha kwa nini?
Weka balbu bwana. Atafanya au asifanye kabisa kwa sababu umemwambia cha kufanya.
2. Wanaume hawapendi mwenzi mwenye makelele, mlalamishiYeye ni kulalamika
kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. Japo wanawake nao wanasema kuna wanaume
walalamishii balaaa. Na wenye gubu wanasusa kula mpaka kuongea wanawanunia
wake zao mmmmh!
3. Wanaume hawapendi mwenzi mchafu Mchafu wa mwili wake na hata
nyumbani kwenye suala la kutunza nyumba wanayoishi. Uchafu hufanya
mwanamke apoteze mvuto.
4. Wanaume hawapendi mwenzi mbishi Japo na wanawake wanasema
wanaume ndio wabishi zaidi. Utampa mwanaume ushauri lakini haufanyii
kazi ubishi mwingi.
5. Wanaume hawapendi kuamrishwa na mwenzi wao Mwenzi mbabe
anaetoa amri na kumtawala hawataki.
6. Wanaume hawapendi kuhisiwa hisiwa na kusachiwa sachiwaKumpekua
kwenye simu, mifuko ya suruali kwamba unamulika mwizi. Hawapendi,
tena pengine hawajafanya jambo la kuwafanya wahisiwe vibaya.