KULA NANASI KWAHITAJI NAFASI!

No Comments
Najua nikisema sana nitaonekana nina mdomo wakati kila kiumbe kina mdomo, lakini kwa vile kuwapasha ndiyo hobi yangu acha niwachane live simuogopi mtu.
Leo nimekuja na makavu kwa waume zetu wanaotutesa kwa raha zao, jamani hivi waliosema kula nanasi kwahitaji nafasi walikosea na raha ya mzuka uache upande usiuzuie ni sawa na kuizuia chafya.
Raha ya chafya iache itoke yote hata haja ndogo yaweza kukutoka kwa utamu wake, asikuambie mtu, ukiiachia ina utamu wake.
Jana nimepata malalamiko kutoka kwa shoga yangu eti mumewe anambania, mmh, makubwa tena watu wazima kubaniana kulikoni? Mmh, majibu kumbe si kwa mambo yetu, bali sehemu ya kulitafuna nanasi haina nafasi.
Basi mwakwetu nikakaa kitako kutaka kujua hilo nanasi kwa nini likose nafasi, kwani tamu ukiiondoa hamu hupoteza utamu. Basi akazidi kunimwagia makavu, mtu mzima mdomo mwaaa.
“Basi shoga nyumba tuliyopanga tuna chumba kimoja na tuna watoto wanne, mwenzangu hatuli nanasi mpaka watoto walale, basi mwenzenu nimekuwa kama mlinzi wa usiku, hamu zikinipanda shuruti nikomae mpaka saa sita au saba za usiku ndiyo nijilie nanasi na mzee mwenzangu.
Siku nyingine nikisubiri kutokana na uchovu wa kazi za kutwa nzima usingizi unanipitia, nikishtuka kumekucha na watoto wameamka, lakini muda huo mzee naye anawahi kazini bora angekuwa anachelewa kutoka tungelianzisha asubuhi.
Yote tisa, kumi shosti wakati huo wa kulila hilo nanasi, mwenzenu siwezi lilia gizani kwa kumuogopa jirani, mume wangu kanitolea mahari kwetu na kilichonileta kwake pamoja na yote, mlo wa nanasi ndiyo hasa unaodumisha ndoa.
Nami nimetoka kwetu, nimefundwa nikafundika najua kumpa mahaba ya maneno tu mume wangu wakati wa kula nanasi yakamtia uchizi.
Kingine siwezi kumnyima sifa zake mume wangu pale atakapolitafuna vizuri nanasi, lazima nimwambie wakati huo wazimu wa mapenzi umenipanda mtoto wa kike humaliza maneno yote kinywani.
Lakini siku hizi imekuwa siyo mzuka ukinipanda tu utamsikia shemeji yako, taratibu mke wangu utawaamsha watoto. Jamani najikuta nikiteseka kushindwa kuonesha uwezo wangu na kuogopa nyumba ndogo kutumia udhaifu huo.
Kuna kipindi mume wangu akinikataza, sikubali najiachia kama gari lililokosa breki katika mlima wa Kitonga na kumueleza akiona kero aongeze chumba kingine. Basi shoga toka nimueleze hivyo amekuwa hataki kunipa haki yangu kwa kisingizio nitaamsha watoto na akinipa nikianza kucharuka anazima muziki mbona nateseka mtoto wa kike.”
Mmh, wote mmesikia na sitaki kuongeza kitu chochote nayaacha hivyo hivyo ila nina kazi na wewe baba unayenikodolea macho. Jamani kila lisemwalo lina maana yake, kula nanasi kwahitaji nafasi na raha ya mzuka ukipanda uachie si kuubana sawa na kuibana chafya.
Kama mna chumba kimoja na uchumi hauruhusu, basi tokeni hata siku moja mwende nyumba ya wageni huko jiachieni mtakavyo mkirudi nyumbani wepesiii hakuna kuamsha mtoto wala kero kwa jirani.
kutoka kwa Anti Nasra Shangingi Mstaafu.
back to top