STAA wa sinema za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amefunguka kifo cha mwigizaji Adam Kuambiana kinampa majonzi zaidi kila anapofikiria muvi waliyocheza kwa mara mwisho na marehemu.
Akieleza masikitiko yake, Davina alisema kabla Kuambiana hajapatwa na umauti, waliigiza naye sinema ya Stupid Farther na Who is My Son akiwa na Mtitu (William) ambazo zote bado hazijatoka.
