JE MWANAMKE UNATAKA KUWA SUMAKU KWA MWANAUME?

No Comments



1.    Mwanamke jipende mwenyewe
Mwanamke ni lazima ujipende na kujiamini na ukigundua kuwa hisia
 zako zaapenzi zimejikita kwa huyo mwanaume ambaye hisia zako
 zinaamini kuwa ni yule ambaye umewahi kumuwaza kuwa ungependa 
kuwa nae basi usieleze kwanza uongo maana akija gundua weeeeee……noma.
Hapa niweke wazi kuwa ni muhimu mwanamke au mwanaume,
 kwa pamoja tujue kuwa tofauti yetu na mbuzi siyo miguu au
 manyoya bali kitu kingine kikubwa zaidi. Kitu hikikikubwa
 ndicho sisi – sisi ni jinsi tunavyofikiri ambapo kwa kufikiri 
kwetu tunakuwa kama tulivyo ambao ndiyo sisi wenyewe.

2.    Jifunze namna ya kuzuga
Sisemi jifunze namna ya kudanganya bali ‘’kuzuga’’ naamini naeleweka
 vema ambapo wanawake wengi wenye kujua kuzuga wamekwa sumaku
 kubwa kwa wapenzi wao ama kwa wabnaume wanaowahitaji.
Wanawake wenye ujuzi wa kuzuga wamekuwa wakifanikiwa kuwanasa
 wanaume wengi kutokana na ujuzi wa kutumia viungo vyao walivyop
[ewa na Mungu huku baadhi wakitumia macho yao kwa kuangaliana 
mara kwa mara na wanaume wanaovutiwa huku baadhi wakitumia 
midomo yao kuilamba kana kwamba anasawazisha mafuta katika
 midomo hiyo.
Mbinu hii inawapagawisha wanaume wengi ambao hujikuta akikuuluza
 jina ama moja kwa moja akakusogelea na kukusabahi na kujitambulisha 
ama kuomba namba yako ya simu, si unajua utandawazi umewapotezea
 wanaume wengi ujasiri wa kutongoza zaidi atakupigia simu, si mnajua 
wengi tunatongozana kupitia simu…si vibaya ingawa hamu inapotea kidogo.

3.    Panga ratiba ya kutoka, ‘’siyo kusaka mabuzi’’
Wanawake wengine wamekuwa wakilaumu kuwa hawatongozwi na
 wanashindwa kuwadaka wanaume wanaowataka kimapenzi huku 
wao wenyewe wakiwa tatizo. Wengi hushinda nyumbani kama
 watoto wa Mfalme jambo ambalo wengine wamejikuta
 wakizeeka na kuanza kukumbuka hata kwa kulazimisha
 kuwa walau nwapate watoto.
Hali hii mwanamke utaiepuka endapo utakuwa na walau na 

ratiba zako nzuri hata kama haupendi kwenda Disko au ni geti kali basi hata
 week end uwe na ratiba ya kutembea ufukweni au mahala ambako unajua kuna 
watu wanajichanganya kidogo majira ya jioni na ahapa sizungumzii kuwa
 unaenda kutafuta soko bali kama unajiamini kuwa unamvuto naamini uchaguzi 
wako utakuwa mgumu kwasababau wengi watatamani kuwa nawe, si 
unaushawishi banaaaa…

4.    Kosoa kwa hekima
Mbinu hii itawasaidia sana wanawake ambao wapo tayari kwenye ndoa
 na mahusiano ya kawaida ambapo kuna mahala wanawake wanajisahau na 
kuwatamkia wanaume wao maneno yasiyo na hekima, kwa mfano utamsikia
 mwanamke anamwambia mwanaume wake kuwa ‘’wanaume wenzako 
wanajenga, wewe kila siku ahadi tu’’ kauli kama hii ni kosa na kasoro kubwa.
Ukiachiliambali kwamba hiyo ni lawama, lakini kauli kama hiyo inajenga 
hisia kwa mwenzako kuwa mwanamke huyu kumbe anapenda kuwa 
na wanaume kama hao hivyo wanaume wengi hawapendi kushauriwa 
bila hekima na kudhani kuwa wanawake hao wanaodhani wanaume 
wao hao siyo wa maana hivyo mwanamke ukitumia maneno yasiyo
 na hekima huwezi kuwa sumaku kwa mwanamume wako.
Kwa leo tuishie hapa wiki ijayo na kuendelea nitakuletea mfululizo 
wa tofauti zetu yaani mwanamke na mwanaume na ujua kuwa 
kutentewa vizuri na mpenzi wako ni haki yako au la na hapo tutaelezana 
madogomadogo yafukuzayo wapenzi.
back to top