BENKI YA CRDB YAZINDUA MFUMO WA KULIPIA MATIBABU KWA KUTUMIA NJIA YA KIELEKRONIKI 'KCMC TEMBO CARD'

No Comments
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB akizungumza wakati wa uzinduzi wa KCMC Tembo Card itakayotumika kwa ajili ya malipo ya matibabu katika hospitali ya KCMC.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya  Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi ya malipo ya KCMC Tembo Card kwa ajili ya malipo ya matibabu katika hospitali ya KCMC badala ya fedha taslimu.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB, wakiwa katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkurgenzi wa benki ya CRDB tawi la Arusha, Chiku Issa na wa pili  kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo Mikubwa, Philip Alfred.
Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya KCMC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akimkabidhi KCMC Tembo Card, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao, itakayowawezesha wagonjwa wanaofika katika Hospitali ya KCMC kulipia huduma za matibabu kwa njia ya kadi badala ya fedha taslimu. Uzinduzi huo ulifanyika mjini Moshi, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Prof. Raimos Olomi.

Mkuuwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao akikata utepe wakati wa uzinduzi wa malipo ya matibabu kwa kutumia kadi ijulikanayo KCMC Tembo Card katika hospitali ya KCMC mjini Moshi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati), akiwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini , Askofu Dk. Martin Shao akilipia huduma za matibabu katika Hospitali ya KCMC kwa kutumia kadi maalum ya KCMC Tembo Card badala ya fedha taslimu, wakati wa uzinduzi wa hudumahiyo uliofanyika mjini Moshi.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao akionesha  kadi ya malipo ya matibabu katika hospitali ya KCMC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akifanya malipo ya matibabu kwa njia ya kadi badala ya fedha taslimu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC, Prof. Raimos Olomi akilipia matibabu katika hospitali hiyo kwa kutumia kadi maalum ya KCMC Tembo Card.
 Dk. Kimei akipanda mti wa kumbukumbu.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Baadhi ya watu wakishuhudia uzinduzi huo.

Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB.

Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa KCMC Tembo Card mjini Moshi.

Dk.Charles Kimei akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya wateja wakubwa wa benki iliyofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, IGP Said Mwema akipata chakula wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC, Prof. Raimos Olomi (kulia) na Mkurugezni wa CRDB, Dk. Charles Kimei wakipata chakula.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu (IGP), Said Mwema (wa nne kushoto), akicheza ngoma za asili za kabila la wachaga wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wateja wa benki hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia), akiwa na Mkurugenzi wa tawi la CRDB Arusha, Chiku Issa wakati wa hafla hiyo. 

MOSHI, Tanzania
BENKI ya CRBD imezindua mpango mpya wa huduma za kulipa kabla kwa kutumia kadi za benki hiyo katika hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi. kwa lengo la kurahisisha malipo yanayotolewa kwa wagonjwa na kuongeza mapato ya hospitali. Kutokana na uzinduzi huo wa kadi hiyo mpya sasa huduma zitaweza kupatika kwa urahisi kwa wagonjwa ambao ni wateja wa benki hiyo watakapokuwa wanapata huduma katika hospitali hiyo. 
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo  Dk Charles Kimei alisema Benki kuongeza na kuboresha huduma zake nchini kwa kasi ili iweze kuwafikishia wananchi wa kila aina huduma hizo ili kurahisisha maisha yao. TemboCard KCMC Card’ sasa itakuwa niKadi ambayo itakuwa ni suluhisho la ukusanyaji fedha za malipo yahuduma katika hospitali hii ya rufaa ya KCM.
back to top