TASNIA ya filamu Bongo imepata pigo tena baada ya msanii aliyekuwa akichipukia kwa kasi, Patrick August ‘Bryton’ kufariki dunia kwa ajali mbaya ya pikipiki.Akizungumza na paparazi wetu, Mwenyekiti wa Sherehe na Maafa kwa wasanii wa Wilaya ya Kinondoni, Masoud Kaftany alisema Bryton alipata ajali usiku wa kuamkia Jumapili maeneo ya Tabata - Relini wakati akirejea kwao maeneo ya Tabata - Kinyerezi.
“Alikuwa akiendesha mwenyewe pikipiki, akavaana uso kwa uso na gari, ilikuwa ni ajali mbaya sana kwani marehemu alipasuka vibaya kichwa hali iliyosababisha damu nyingi kuvuja na kusababisha kifo chake,” alisema Kaftany.
Baadhi ya sinema alizoigiza enzi za uhai wake ni pamoja na Muuza Genge na Mapenzi ya Fukara iliyomshirikisha Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wasanii wengine.
Mwili wa marehemu Bryton ulisafirishwa jana (Jumanne) kwenda Rombo, mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyikwa leo Jumatano.
Mwili wa marehemu Bryton ulisafirishwa jana (Jumanne) kwenda Rombo, mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyikwa leo Jumatano.