AUNT AKINUKISHA...

No Comments

KAMA hakuwahi kutoa sadaka, huu ndiyo muda wake! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson anadaiwa kukinukisha nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu baada ya kunusurika kufumaniwa na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo a.k.a Moze Iyobo ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson akiwa na shost yake Wema Isaac Sepetu.
Habari zisizokuwa na shaka zinadai kwamba tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo Aunt alisababisha tafrani iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Mwengi Ally.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana, Mwengi alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo timbwili lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar.
Ilidaiwa kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla waliibuka wasichana saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao walidadavua kwamba katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa peke yake, angeumizwa Aunt alikimbilia  nyumbani kwa shoga yake, Wema.
Ilidaiwa kwamba wasichana hao hawakuishia hapo kwani walimkimbiza Aunt hadi wakamuona akiingia kwa Wema ambapo walipofika getini walikutana na meneja wa msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Mirrow, Petit Man ambaye walimuomba amtoe Aunt ili wamshikishe adabu ajifunze kukaa mbali na waume za watu.
Ilisemekana kwamba katika tafrani hiyo getini, Wema alitoka na msichana wake aitwaye Careen lakini Aunt hakutoka ambapo waliwaambia wasichana hao kuwa Aunt hawezi kutoka na isitoshe wa kulaumiwa ni Moze Iyobo kwani yeye ndiye anayedaiwa kumtongoza Aunt na kuanza kuchati naye hadi mkewe akanasa meseji zao za mapenzi.
Baada ya kujazwa data hizo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mwengi ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikiri kwenda kwa Aunt na Wema lakini hakufanikiwa kumpata Aunt kwani kama angemkamata, maafa yangetokea.Mwengi alisema kuwa siku ya tukio aliitwa na Aunt maeneo ya Mlimani City, Dar na akamwambia aende na mtoto akamfanyie shopping.
Alisema baada ya kuambiwa hivyo hakuwa na hiyana kwani alijua kuwa ni kama mama yake mkubwa na shoga wa mpenzi wa baba yake mkubwa ambaye ni Diamond, kumbe nyuma ya pazia kulikuwa kuna kitu kingine kimejificha.“Niliporudi nyumbani, mume wangu aliniambia nimpige picha kwa kutumia simu yake, nilipoifungua ndipo ikaingia meseji kutoka kwa Aunt.
“Nilipoisoma ile meseji nikagundua kuwa walianza kuchati muda mrefu kuhusu mapenzi yao, ndipo nikakusanya jeshi langu na kumfuata nyumbani kwake nikamshikishe adabu, amshukuru Wema kumficha maana sipati picha kwa jambo ambalo lingetokea. Ingekuwa mwisho wake wa kupora waume za watu,” alisema Mwengi.
Alipotafutwa Aunt na kuulizwa juu ya sakata hilo, alijibu kwa kifupi: “Sina muda mchafu wa kuongea halafu nimelala, kwa sasa niache nipumzike.”
back to top