MBWA WAKE MNYORORO KAMBA UNAMUONEA

No Comments


Hehehehe! heheheeeeee acha nicheke mie mwana wa kizibo, mjukuu wa
mdomo wa chupa. Nimepigiwa simu na mashosti zangu eti somo nililotoa wiki iliyopita limewasaidia, sasa hivi wanakula kitu kamili siyo msosi wa kuungaunga.
Sasa hivi safari ikianza pamoja wanamaliza pamoja. Siyo kila siku kuteremshiana njiani na kukuacha utembee kwa miguu, nani alikuambia hapendi raha.
Leo nataka kuwaeleza kitu kimoja kuhusu waume zetu, unajua kuna vitu huvifanya kwa mazoea kwa vile mkewe basi, utajijua, ufike usifike shauri yako. Nasi tusiwachekee kwa kuwaachia watufanye watakavyo, kwa kutuacha njiani na kutufanya tutafute njia mbadala kufika mwisho wa safari.
Kazi yetu kupinda midomo kama pindo la jamvi na kumuacha mwenzako anamwaga mzigo kisha taratiiibu anateremka, unamuangalia tu michozi mwaaa,  mbayaaaaa eeeh.
Wewe nani kakwambia kuna mtu hulia msiba kwa kushika kichwa cha mwenzake, kila  mlia msiba hushika kichwa chake, nawe unategemea kilio chako ulie na nani kama siyo  peke yako?
Leo lazima nikupe ubunifu wa kufika mwisho wa safari, ukimuona mwenzako kashusha mzigo nawe bado, usikubali kumuachia, lazima umwoneshe kuwa hujafika, mshike kiuno, mrudishe mwambie mwenzio bado kabisa.
Unafikiri kupinda mdomo kunasaidia nini maji ya moto yatakukomaza bure na kukutia sugu upoteze ladha halisi ya maji ya kisima.
Nawe mwanamume hivi kweli umemuoa mwenzio hata hujali mateso yake?
Hivi kweli wanajua hali ya mwanamke katika tendo,  wanajua anataka nini hasa wawapo katika kilimo cha matuta. Waswahili wanasema siku zote mchuma janga hula na wa kwao, sasa mbona janga uchume wewe nile mimi?
Ni wazi hata waume zetu wapo wasiojua kama wenza wao nao wanatakiwa wafike mwisho wa safari au kujua kama mwenzie amefika au bado. Japo mimi ni mwanamke, lakini leo nawapasha tena mpashike sichagui sibagui siku zote raha ya wimbo kupokeza.
Siyo uimbe peke yako mwenzio kama anaumwa jino, kazi yake kugugumia kama kakanyagwa kwenye kidonda, najua si wanaume wote wataalamu wa mambo fulani, wengine hujua raha ya mapenzi ni kumwaga mzigo na kuteremka juu ya mnazi.
Lazima umsome mwenzako, hasa katika safari ya kuelekea kisiwa cha utamu usioisha hamu.  Siku zote sisi wanawake tuna aina zetu za kufurahia safari, wapo wanaohema kama wana pumu na mwisho wa safari utasikia pumzi zake zinakwenda kwa kasi, akitulia ujue keshafika huyo.
Mwingine hupiga kelele kama kaonewa au kumaliza maneno yote mdomoni na akiiona pwani hukujulisha kabisa kuwa chombo karibu kitatua nanga bandarini. Nawe hapo lazima uzidishe kasi ili kuhakikisha chombo kinatua nanga salama.
Hii itazidisha upendo na kuwafanya wake zenu mwisho wa safari watoe asante na si kugeuka na kukupa mgongo huku mdomo umeupinda kama pindo la jamvi. Sifa ya mwanaume si kumlisha mkewe na kumvisha, yote huwa tisa kumi ni pale hakimu akipanda juu ya meza ya hukumu kuhukumu kulingana na kosa.
Siku zote mbwa wake mnyororo kamba utamuonea. Siyo kaiba kuku umfunge miaka kumi na mwizi wa ng’ombe wiki moja, usimuonee huruma katenda kosa hilo akitegemea hukumu stahiki.
Usimuache mkeo njiani, ona aibu mwanaume usiyemfikisha mkeo unamuacha nani amfikishe au unamlazimisha atafute wa nje? Jisikie fahari mwisho wa safari mkeo akuambie mpenzi hakika leo umejua kunipa raha zisizo mfano. Ni hayo tu!
back to top