BIFU? Komediani Haji Salum ‘Mboto’ amekanusha vikali kuwa na bifu na Wema Sepetu baada ya tetesi za chinichini kuvuma kwamba wapo kwenye bifu zito.
Akijibu tuhuma hizo, Mboto alisema kuwa haoni sababu ya kuwa na bifu na Wema zaidi ya kushirikiana naye katika kazi na hivi karibuni amempa kazi ya kumuandikia stori na makubaliano yao yalikuwa mazuri.
“Dah! Bifu na Wema? Naanzaje kwanza? Aisee Wabongo kwa kuzusha vitu wamejaliwa, nashangaa kwani hakuna kitu kama hicho na hakijawahi kutokea,” alisema Mboto.Komediani wa Bongo, Haji Salum ‘Mboto’.
“Dah! Bifu na Wema? Naanzaje kwanza? Aisee Wabongo kwa kuzusha vitu wamejaliwa, nashangaa kwani hakuna kitu kama hicho na hakijawahi kutokea,” alisema Mboto.Komediani wa Bongo, Haji Salum ‘Mboto’.
Hivi karibuni, mitandao mbalimbali ya kijamii ilieneza habari kuwa wawili hao ‘hawaivi’.