KUTOKA moyoni? Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa siku zote amekuwa akimuombea dua shosti wake, Wema Sepetu ‘Madam’ na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ uhusiano wao udumu.
Aunt alifunguka hayo mara baada ya kuulizwa na mwanahabari wetu juu ya mtazamo wake kuhusu mapenzi ya wawili hao ambapo alisema mapenzi yao yamekuwa yakimvutia na kila mmoja anaonekana kuwa na mapenzi ya kweli kwa mwenzake hivyo hawezi kupendezwa hata siku moja akiona hawapo pamoja.
“Kusema kweli naona hawa watu wanapendana na kujaliana sana, siku zote nawaombea kwa Mungu mapenzi yao yadumu milele na ninaamini watafikia malengo yao, sitapenda hata siku moja kuona wapo tofauti,” alisema Aunt.