DI MARIA ASAINI MIAKA 5 MAN U

No Comments
WINGA Angel di Maria amejiunga rasmi na klabu ya Manchester United kwa ada ya pauni milioni 59.7 kwa mkataba wa miaka mitano.

Angel di Maria akipozi na Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal.
Di Maria amekamilisha usajili huo leo usiku na atakuwa akilipwa pauni 200,000 kwa wiki nyuma ya Wayne Rooney anayelipwa zaidi klabuni hapo.
Staa huyo aliyetokea Real Madrid amevunja rekodi ya Ligi Kuu ya England kwa uhamisho wake wa bei ghali.
Di Maria akiwa na jezi ya Man U.
Baada ya kukamilisha usajili huo, Di Maria alisema : 'Manchester United ndiyo klabu pekee ambayo ingeweza kunifanya niondoke Real Madrid'
Di Maria anaungana na wachezaji wengine wapya klabuni hapo kama Marcos Rojo, Ander Herrera na Luke Shaw.

back to top