UHURU PENZINI HUONGEZA RAHA

No Comments
Jamani leo nimewaletea shangingi wa kiume ambaye mli-mmisi muda mrefu. Kwa vile kapita anga zangu nimempa kesi moja aijibu kwa vile inagusa upande wake. Babu Poa uwanja ni wako si unajua mimi huwa sirembi kamua mwanaume.
“Asante Anti Naa, nina imani wengi tunajua baada ya kuandaa chakula na kuanza kula kuna kitu muhimu sana ambacho wengi huwa tunakisahau. Naona macho yashakutoka kutaka kujua mnasahau nini.
“Jamani uhuru ndani ya mapenzi ili wote mfurahie chakula chenu. Najua unauliza uhuru gani huo?
“Katika pitapita yangu, nimepata malalamiko mengi kutoka kwa wanawake ambao siku zote hufanywa chombo cha starehe na kunyimwa uhuru wa kuzungumza wakati wa mchezo, hufikia hatua hata kama amechoka anaogopa kukaripiwa, hata kuambiwa huenda mchana amemhujumu kwa kutembea na mtu mwingine, Ooh! Hapana haiendi hivyo!
“Kwanza lazima ujue safari ya mahaba inataka nini. Safari ya mapenzi si ugomvi au raha za upande mmoja, unapojisikia unatakiwa utimiziwe hata kama mwenzio anaumwa. Hii hufanya hata mwanamke apoteze hamu ya mapenzi, kila akuonapo, hata mnapokuwa kwenye dimbwi la mahaba anakuwepo-kuwepo tu, si kulifurahia bali kutimiza wajibu kwa mumewe au mpenziwe!
“Mapenzi maana yake ni upendo, furaha, tulizo la moyo, kato la kiu ya mwili. Mapenzi ni raha ya pande mbili, mapenzi ni kuoneana huruma, ni kuona mwenzio akiondokewa na mawazo na majonzi. Mfanye mwenzako alifurahie lako, alikumbuke uwapo mbali.
“Mpe uhuru ili akupe penzi kutoka chini ya uvungu wa moyo wake, mwache alie kilio cha fuhara siyo kile cha maumivu, wewe na mpenzio kila mmoja ana uhuru wa kufanya atakavyo katika mwili wa mwenzie bila kulazimishana bali kwa kuridhiana, kitu kinachowafanya kila mmoja ajisikie raha na furaha!
“Kila kiumbe kina udhaifu wake mnapokuwa kwenye sita kwa sita, hasa wanawake kila mmoja ana namna yake ya kujisikia na kuonesha alivyoguswa sehemu zake, wapo wanaolia utafikiri wameonewa, maskini kumbe raha zimemzidi, wengine huongea kama wamemeza CD ya maneno, wengine utafikiri si muda mrefu watakufia kwenye kilinge, pumzi zinawatoka kama wagonjwa wa pumu, mwingine kiini cheusi cha jicho huwa hakionekani!
“Yote hayo ni kutokana na kuwa huru na kuweza kufanya alichonacho bila uwoga.  Ifike hatua wanaume tubadilike, Oooh! Nimekumbuka kuna mtu amenitonya eti wanaume wengine huwa wakali kwa kuwa mambo mengi ya mahaba hawayajui.
“Lakini kama tupo pamoja toka mwanzo nina imani  sasa mwanaume wa aina hiyo ataweza kumfurahisha mpenzi wake bila ngumi wala lugha kali.
Hakuna aliyezaliwa akijua, wote tumejifunza kupitia njia hizi au kuuliza kwa wenzetu, usione aibu kuuliza kwa mwenzio, nina imani kama anajua hawezi kuwa mchoyo atakupa elimu hii kwani ni ya bure.
“Hata wewe una uhuru wa kumpa mwenzio, naye ajikute siku moja chozi limemtoka kwa raha za ajabu ambazo hajawahi kuzipata tangu aingie kilingeni. Nina imani nimeeleweka, tukutane wiki ijayo kwa mada mpya, nakutakieni mapenzi yenye utamu usiyoisha hamu. Kwako anti Naa.”
back to top