LISTI ya mastaa inazidi kuongezeka kuelekea Tamasha la Usiku wa Matumaini, linalotarajiwa kufanyika Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo burudani kabambe kutoka kwa wakali wa muziki wa Bongo, Juma Nature, Madee, Roma Mkatoliki, Ali Kiba, Meninah na wengine kibao watadatisha mashabiki na kuacha historia katika burudani.
Roma atakuwa wa kwanza kulitikisa jukwaa kwa kuachia ngoma zake zote kali zinazotikisa katika anga la burudani ikiwa ni pamoja na 2030, Kidole cha Mwisho, Mathematics, Pastor na Karibu Kwenye Karamu (KKK), kisha Rais wa Manzese, Madee, atamaliza kila kitu jukwaani kwa ngoma zake kali kama Tema Mate Tuwachape, Historia, Hip Hop Haiuzi, Pombe Yangu na nyingine nyingi.
Baada ya wakali hao kushuka, msanii asiyechuja, Juma Nature ‘Kiroboto’ na timu nzima ya TMK Wanaume Halisi, watakuwa na jukumu la kuendeleza moto wa burudani kwa kuporomosha nyimbo kali kama Mgambo, Hakuna Kulala, Tatu Bila, Ndege Tunduni na nyingine kibao.
Mbali na burudani hiyo, kivutio kikubwa kitakuwa mchezo wa mpira wa miguu kati ya Wabunge wanaoishabikia Yanga ambao wanang’ara na usajili wa Ridhiwani Kikwete, dhidi ya wenzao wa Simba wanaoongozwa na golikipa mahiri ambaye pia ni Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan.
Masumbwi
Bondia anayeshikilia Mkanda wa UBO, (Universal Boxing Organization), Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’, atachapana makonde na mpinzani wake ndani na nje ya ulingo ambaye ni bingwa wa zamani wa Afrika Mashariki na Kati, Mada Maugo, ‘Mbunge mtarajiwa’. Ikumbukwe kuwa mabondia hawa walikutana Agosti 30, 2013 ambapo Maugo aliangukia pua kwa kuchezea kichapo, hivyo kuahidi kulipiza kisasi katika tamasha hili.
Kabla ya hapo, kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo msanii wa muziki wa dansi, pia bondia, Khalid Chokoraa, atazichapa na Said Memba huku Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangala, akipanda ulingoni kuonyeshana ubabe na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, wakati mastaa wa Bongo Movie, JB na Cloud, wakimaliza utata wa nani mbabe ulingoni.
Alade vs Shilole
Ni mtifuano wa aina yake pale staa wa Johnny kutoka Nigeria, aliye katika chati kwa sasa, Yemi Alade, atakapoonyeshana kazi na mkali wa Chuna Buzi, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ili kukonga nyoyo za mashabiki watakaojitokeza siku hiyo.
Soka
Utamu mwingine wa Tamasha la Matumaini ni pale mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar, watakapoumiza nyasi kwa kuumana na mabingwa wapya, Azam FC, ambapo kila timu imeahidi kushusha ‘skwadi’ yake ili kuangalia upungufu uliopo kabla ya Ligi Kuu Bara kuanza.

Usiku wa Matumaini ni tamasha kubwa ambalo hutumika kuwaunganisha Watanzania na kuhusisha burudani tofauti kwa kuwakusanya mastaa kibao kutoka ndani na nje ya nchi katika jukwaa moja huku asilimia 20 ya mapato yake ikichangia mamlaka ya elimu. Mwaka jana mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete.
Burudani yote hii inaletwa kwenu kwa udhamini wa Vodacom, E-FM, Times FM, Clouds FM na Azam TV. Hii si ya kukosa!!!!!!!!!
Burudani yote hii inaletwa kwenu kwa udhamini wa Vodacom, E-FM, Times FM, Clouds FM na Azam TV. Hii si ya kukosa!!!!!!!!!