



TIMU mbili za Afrika zilizokuwa zimebaki katika Michuano ya Kombe la Dunia linaloendelea nchini Brazil, Nigeria na Algeria nazo zimeyaaga mashindano hayo. Katika mechi ya kwanza Nigeria walikubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa timu ya Ufaransa huku Algeria akipigwa 2-1 na Ujerumani. Kwa matokeo hayo, Ufaransa na Ujerumani zitakutana Robo Fainali Julai 4 mwaka huu.