Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Wimbo wa Tuulinde Muungano uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana ambapo pia alimfagilia msanii Diamond kwa juhudi zake.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wasanii baada ya uzinduzi huo.
Mama Maria Nyerere akiwasili katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Wimbo wa Tuulinde Muungano.
Godzilla akifanya makamuzi wakati wa uzinduzi huo.
Madee akiwapa raha wananchi wakati wa uzinduzi wa Wimbo wa Tuulinde Muungano jana.
Shilole akiwapa raha mashabiki.
Wasanii wakiwasalimia wananchi katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana.