unazijua stress za wasanii wa Bongo?

No Comments

Kati ya vitu ambavyo kwa msanii wa hapa bongo anavyojali most,miongoni
mwao ni ku-maintain status yao ya u-superstar,na moja kati ya vitu anavyotakiwa
kufanya mtu kama star ni kufanya vitu tofauti kabisa na mtu wa kawaida .
 Kwa bongo muziki umekua ukianza kulipa na pale msanii anapopata
pesa hivi ndio vitu ambayo msanii wa kibongo hupata stress from:-
usafiri ,Wasanii wa bongo huumiza vichwa wanunue gari gani ili wawe
kama msanii fulani au waongeze status yao. Kwa wale wasanii wadogo
 stress zikizidi baadhi Yao hudiriki hata kukodisha magari ya
 Watu na kulipa kila mwisho wa mwezi,ili tu wasionekane
 wakipanda daladala,tu naweza kukubaliana kuwa si kila
msanii hapa bongo anauwezo wakumiliki gari kutokana tu
na mauzo ya Kazi zake,cause hata underground aliyetoka
na ku-hit na nyimbo moja redioni utakuta naye anahangaika na
Mishe za kutaka ku-maintain status.

Mavazi , Usishangae kuona hata Nguo Watu wanagongea katika
harakati tu za kuonekana unique,cause am sure si kila celeb hapa
 town anauwezo waku-change dress code kila siku,and Kati ya
 vitu ambavyo vinaongeza stress zaidi ni ujio wa instagram,social
network ambayo kila celeb huwa anajitahidi ku-update Picha Y
ake bila ya kuonekana Kama Amerudia Nguo,cause fans
 lazima waliongelee Hilo, hivyo kutengeneza story mpya ya
 town ambayo is nzuri kWa mtu maarufu.
mavazi copyright www-vibe-co-tz

Nyumba, Siku za karibuni tumeona wasanii kibao wakionesha nyumba
 zao walizojenga na hili swala linatokana na stress wanazozipata pale
wanapoona wasanii wengine wanajenga nyumba na wengine sio moja
 tu bali zaidi ya moja. Kwa siku za kaaribuni wasanii wengi wameonesha
 nyumba zao walizojenga kwa mfano linah , young D ,
Barnaba na Diamond. Muziki kwa sasa unalipa na hii stress
ya nyumba itazidi kuongeneza kadiri siku zinavyoendelea.

Nyumba copyright www-vibe-co-tz

Miili Mizuri , Hiki ni kitu kikubwa na kigumu kwa wasanii wengi.
Msanii ni kioo na hamna msanii anayependa kuonekana akiwa na
umbo baya kwahiyo wengi siku hizi hutumia muda wao kwenda gym
 kuweka miili yao sawa huku wengine wakiwa na personal trainers kabisa.

Gym copyright www-vibe-co-tz
back to top