Mshahara wako wa kwanza
kawaida ndio mshahara mdogo kabisa utakaopata lakini unakujaza msisimko na furaha sana na kujiona mtu wa pekee.

Kuendesha gari peke yako mara ya kwanza
Kuendesha gari unaweza kuchukulia poa lakini unakumbuka mara ya kwanza umeendesha gari peke yako, ile hisia ya “duh ! ninaendesha gari peke yangu” , surely ni bonge la moment maishani.

Graduation
Sio tu kwamba umefanikiwa kumaliza elimu yako baada ya miaka mingi bali the fact that marafiki,wazazi na watu wako wa karibu wamekuja kukupa support ni tukio moja muhimu sana.

Mazungumzo ya kiutu uzima na wazazi wako
Kuna muda utafika wazazi wako hawatakua tena watu wakuweka sheria na kukubana bali wanakua watu wa rika yako.Wazazi wanapamua kuongea na wewe juu ya mategemeo yao kwako na kukupa mafunzo ya maisha ni muda ambao umakini unaitajika na ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako.

Safari na marafiki zako
Kuna kipindi kinafika unakua very busy so unapopata muda wa kusafiri na rafiki zako inabidi uthamini muda huo.

Kufanya vitu mwenyewe
kuna kipindi unahitaji muda mwenyewe. hivi ushawahi kutoka kwenda sehemu mwenyewe? kama ujawahi basi ujaribu maana utajisikia vizuri kuliko.

Falling in love
love inakua na kuongezeka kwenye mahusiano bora. Lakini hamna kitu cha msisimko na furaha kama mara ya kwanza unapofall in love. inabidi utunze tukio hili kwenye diary au kitabu sababu siku moja utakumbuka ilivyokua na utakua mwenye furaha.

Kufanya kitu usichotegemea
kitu ulichofanya ambacho kamwe haungefanya.ku-appreciate vitu hivi ni vyema sababu ni mara chache sana maishani utakuja kufanya vitu kama hivi.

Kuondoka Nyumba ya familia
ni watu ndio wakuwajali maishani sio sehemu wanayokaa lakini kwa nyumba ya familia ni tofauti.ukiwa unahama inabidi uache kufanya kitu chochote,tembea chumba hadi chumba na ujikumbushie good times ulizokua nazo kipindi hicho.

Kufanikiwa kazini
Labda ni kufanya mauzo ya kuwe sana kazini kwako au kutengeneza kitu kwa mara ya kwanza inabidi ku-enjoy moment hiyo ikitokea.
