Beyonce na Rihana, kuzua gumzo tena duniani…

No Comments

collagennnnn
Baada ya muda kupita toka rumors za Jay-z kutoka na Rihana wakati huo huo, Beyonce akiwa ndiye mmiliki halali, hii tena lingine ila kwa sasa wakutana wakilinganishwa katika moja ya majarida maarufu nchini marekani, ni baada ya Beyonce kutokea katika cover la jarida maarufu duniani la TIMES, akiwa ametajwa kama mmoja wa watu maarufu wenye ushawishi duniani, huku nyuma  Rihanna nae kutoka kivyake kabisa kwenye jarida maarufu Duniani la Vogue katika toleo la huko nchini Brazil,huku watu mbali mbali wakijiuliza imetokea bahati mbaya au ilikuwa makusudi kwa wawili hao kutoka kwenye msimu mmoja.
collagejjj
Kutokea hivyo kwa pamoja katika sura za mbele za majarida hayo, kumeongelewa kama mashindano fulani hivi, wengi wakiongelea kuhusu, nani haswa ametokelezea kwenye majarida hayo, huku kibiashara kila muandaaji wa majarida hayo akiwa anawaza ni nani atauza zaidi ya mwenzake, hii ni ushindani wa kibiashara tu, ambao umesemekana kufanywa na waandaji wa majarida hayo, ikiwa wao ni kati ya wasanii wa  muziki duniani wenye ushawishi mkubwa wa kufanya watu wasome habari zao, hivyo kutarajia  kufanya  mauzo kuongezeka maradufu zaidi kwa majarida hayo
back to top