
Tamaa ya kutaka kufanikiwa maishani imeenea duniani kote. Hali imebadilika sana,
jinsia ya kike inataka kujitosheleza kwa kila kitu. Lakini mabadiliko ya kibaiolojia
yanabaki vile vile mfano kuzeeka nk. Mafanikio wanayowaza wengi ni utajiri wa
pesa na elimu kubwa. Hii imesababisha wanawake wengi kusoma sana na kufanya
Wengi wanashtuka ikiwa umri wao ni zaidi ya miaka 30, ndio wanakuwa na tamaa ya
kuzaa. Kuchelewa kwao kuzaa kunaweza kuwa kwa taabu ama kuzaa watoto wenye
matatizo mengi ya kiafya.
Kwa miaka mingi, wataalamu wengi wa afya ya uzazi bado wanaamini miaka 20-35
ndio umri sahihi kushika mimba na kuzaa. Pia, wengi wakifikiri matatizo mengi ya
uzazi huongezeka baada ya miaka 35 na
huwa zaidi baada ya miaka 40. Kwa wenzi wawili wanaoishi pamoja,
kuchelewa kuzaa huathiri pia wenza wa
kiume, ambapo mbegu za uzazi za
mwanaume hudhorota kila mwaka upitao
na watoto wamaotokana na wanaume
wazee huwa na hatari zaidi ya kupata
matatizo ya akili na matatizo ya chembe za
urithi.
KUBALEHE
Kubalehe ni hatua muhimu sana lupotia ili
kuweza kuzaa. Wastani wa kubalehe na
kuvunja ungo kwa wasichana ni miaka
9-12 kwa sasa, ingawa miaka ya zamani
ilikuwa kuanzia miaka 12-14.
Baada ya kubalehe binti anakuwa na uwezo
wa kushika mimba, japokuwa uwezekano
huongezeka zaidi kati ya miaka 20-30,
baada ya hapa uwezekano huanza
kupungua.

Kulingana na The American College of
Obstricians & Gynecologists uwezo wa
wanawake kuzaa hupungua katika umri wa
miaka 32 na hupungua kwa kasi zaidi
katika umri wa miaka 37.
Uwezo wa wanawake kuzaa hupungua vile
umri unaongezeka kwa kuwa wanawake
wanapobalehe wanakuwa na idadi kamili
ya mayai katika ovari zao. Namba hii
hupungua vile mwanamke anavyozeeka. Pia
mayai hayazalishwi kiurahisi kwa
wanawake wenye umri mkubwa
ukilinganisha na mabinti wadogo.
Kulingana na National Institute for Health &
Clinical Excellence (NICE) ya Umoja wa
madola (UK), kwa wanawake wenye miaka
35, ni wanawake 94 kati ya 100 wanaweza
kupata ujauzito wakifanya ngono kwa
ukawaida ndani ya miaka 38, ni wanawake
77 kati ya 100 wanaweza kushika ujauzito.
Magonjwa ya njia za uzazi kama
Endometriosis na Uterine fibroids
yanawatokea zaidi wanawake wenye umri
mkubwa ambayo husababisha mwanamke
kutoshika mimba.
Wanawake wenye umri zaidi ya miaka 35
wanaoamua kushika ujauzito wanakabili
hatari ya kupanda kwa shinikizo la damu.
Kupanda kwa shinikizo la damu wakati wa
ujauzito huathiri kondo la nyuma (Placenta)
ambalo hutoa lishe kwa kijusi (kitoto kilicho
tumboni) hali ambayo huathiri moja kwa
moja ukuaji wake.
Pia, hatari ya kupata kisukari kwa
wanawake wanaoshika ujauzito wakiwa na
miaka 35 na zaidi, huongezeka sana.
Kisukari kipindi cha ujauzito huongeza
hatari ya kutoka mimba (Miscarriage), kuzaa
mtoto mwenye kasoro au kuzaa mtoto
mkubwa kupita kiasi.
TAFITI YA HIVI KARIBUNI
Jambo la kushtusha, ni matokeo ya utafiti
uliofanyika Sweden, watafiti wanadai hatari
ya matatizo ya uzazi huanza mapema tu
pale mwanamke anapofikisha miaka 30.
Utafiti uliochapishwa kwenye jarida la
magonjwa ya uzazi (Journal of Obstetrics &
Gynacology) uliofanywa na watafiti kutoka
Taasisi ya Karolinska ya nchini Sweden
umegundua katika nchi tajiri duniani
wanawake huzaa wakiwa na umri mkubwa
kitu kinachopelekea kuongezeka kwa hatari
ya kuzaa watoto njiti (Preterm birth), ukuaji
hafifu wa vichanga na kuzaa watoto wafu
(Stillbirth).
Ili kubainisha hatari kati ya makundi tofauti
ya umri ya wanawake wanaozaa kwa mara
ya kwanza, watafiti walitumia takwimu za
vizazi toka hospitali za Sweden na Norway,
zilizokusanya taarifa za karibu wanawake
milioni moja, kati ya mwaka 1990 na 2010.
Hatari ya kuzaa watoto njiti (Premature
birth) na kuzaa watoto wafu huongezeka
kuanzia miaka ya 30 ingawa toka zamani,
miaka 35 ndio ilitambulika kuwa mwanzo
wa hatari kwa wanawake kupata watoto,
lakini utafiti huu mpya unataja mwanzo tu
wa miaka 30 hatari ya kupata matatizo
katika uzazi huanza.
Kwa kulinganisha kati ya kundi la umri wa
miaka 25-29 na 30-34, wanawake wa
miaka 30-34 wenye mimba za kwanza
walikuwa na hatari ya kuzaa watoto njiti
kwenye wiki 22-31 za ujauzito au kuzaa
watoto wafu.
Kikosi cha watafiti kiligundua pia sababu
zingine zinazoweza kuleta matatizo ya uzazi
mfano wa sababu hizo ni kama kuvuta
sigara au kuwa mnene kuliko kawaida.
Ulla Waldenstrom, profesa wa kitengo cha
afya ya wanawake na watoto katika taasisi
ya Karolinska alisema : 'Tumeshangazwa na
kuongezeka kwa hatari za uzazi katika umri
mdogo sana.'
Prof. Waldenstrom aliendelea ; 'Wanawake
wanaweza ona hatari ni ndogo ila kwa
jamii kiujumla kuna idadi kubwa ya
matatizo yasiyo ya lazima kwao wanawake
wanaozaa baada tu ya miaka 30. Hivyo
nashauri wanawake na wanaume wapewe
taarifa mashuleni juu ya umuhimu wa umri
katika uzazi.'
Alipoombwa ushauri kwa wanawake
wenye umri zaidi ya miaka 30 wanaotaraji
kuzaa, Prof. Waldenstrom alisema ; 'Ushauri
bora ni kuepuka uvutaji wa tumbaku/sigara
na kuepuka unene, kama inawezekana.'
'
KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI (MENOPAUSE)
Wataalamu wa afya wanasema kwamba
mwanamke amekoma hedhi anapokosa
kupata hedhi kwa miezi 12 mfululizo. Ni
wanawake wachache hukoma kupata
hedhi ghafula, yaani, wanakosa hedhi
mwezi mmoja unakuwa mwisho wa
kuipata.

Wanawake wengi huanza kipindi hiki
wakiwa na umri wa miaka 40 na kitu, lakini
kwa wengine huanza wakiwa
wamechelewa wakiwa na miaka 60 na kitu.
Kutokana na mabadiliko ya kiwango cha
homoni kinachotokezwa, huenda
mwanamke akakosa kupata hedhi pindi
kwa pindi, akapata hedhi wakati ambao
hakutarajia au akavuja damu nyingi isivyo
kawaida wakati wa hedhi. Pia huenda
mwanamke akashuka moyo, hisia zake
zikabadilikabadilika na hilo linaweza
kumfanya alielie bila sababu, na pia asiwe
makini sana na asahau mambo.
Kipindi cha kukoma hedhi huwa tofauti
kwa kila mwanamke. Dalili zinaweza
kuonekana kipindi hicho ni pamoja na joto
la ghafula mwilini, ambalo huenda
likafuatiwa na kuhisi baridi. Dalili hizo
zinaweza kumfanya mtu akose usingizi na
kuishiwa na nguvu.
Baadhi ya wanawake hupatwa na joto la
ghafla mwilini kwa mwaka mmoja au miaka
miwili wakati wa kipindi hicho cha kukoma
hedhi.
Wengine hupatwa na hali hiyo kwa miaka
mingi na wachache sana husema kwamba
wao hupatwa na joto la ghafula mara kwa
mara maisha yao yote.
Ni busara mtu afanyiwe uchunguzi wa
kiafya kabla ya kuamua kwamba joto la
ghafula linasababishwa na kukoma kwa
hedhi. Kwa kuwa kuna matatizo mengine
ya kiafya yanaweza kuleta joto la ghafula
mfano ugonjwa wa dudumio, malaria,
homa ya matumbo n.k
JINSI YA KUISHI VIZURI KIPINDI HICHO
Mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza
kupunguza baadhi ya matatizo hayo mfano
kuacha kuvuta sigara, kupunguza au hata
kuacha kunywa vileo, vinywaji vyenye
kafeini na vyakula vyenye sukari au vikolezo
ambavyo vinaweza kusababisha joto la
ghafula mwilini.
Kufanya mazoezi husaidia sana kupunguza
matatizo yanayohusianishwa na kukoma
kwa hedhi. Kwa mfano, mazoezi yanaweza
kupunguza kukosa usongizi na kusaidia
kuboresha hali ya kihisia na pia huimarisha
mifipa na afya ya mtu kwa ujumla.
Ili kumsaidia mwanamke kukabiliana vizuri
na kipindi hicho cha kukoma kwa hedhi,
huenda madaktari wakampa homoni,
vitamini na madini, na dawa za kutibu
kushuka moyo.
Pia ni jambo la busara kuwaambia
uwapendao hali unayokabili ili
wakuonyeshe upendo na wakupe msaada
unaouhitaji wakati wa hali yako.
Kipindi hicho kinapokwisha, wanawake
ambao hutunza afya yao, wanapata tenanguvu
na kuendelea kufurahia maisha.
Asanteni sana kwa kufuatilia