WIKI iliyopita Wema alisimulia mpaka kwenye uhusiano wake na aliyekuwa mwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Chaz Baba. Alisema katika wapenzi wake wote, mwanamuziki huyo alikuwa kipenzi cha dada yake ambaye hakumtaja jina.
Diva wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu.
Pia, Wema alianika kisa cha kuachana na Chaz Baba kwamba ni tabia yake ya ‘umende’. Akatua kwa Diamond ambapo mapenzi yakawa motomoto.
Wiki hii tunaendelea…
Wiki hii tunaendelea…
Mwandishi: Lakini Wema umeongea kote, mbona hujamzungumzia kijana mmoja anaitwa Jumbe Yusuf Jumbe ambaye nakumbuka alikuwa mjasiriamali. Mlikutana vipi na kwa nini mlimwagana? Wema na wewe bwana!
Wema: (uso wa umakini) kwanza Jumbe sijui ilikuwaje!? Lakini kwa wakati ule naweza kusema nilijikuta nikimpenda kwa moyo wote baada ya kuamua kumpenda nikiwa nimetoka kuachana na Kanumba.
“Jumbe nilianza naye uhusiano mwaka 2009. Sitaki kumsema vibaya Kanumba, lakini Jumbe ndiye mwanaume aliyeweka historia tofauti ya maisha yangu.”
“Jumbe nilianza naye uhusiano mwaka 2009. Sitaki kumsema vibaya Kanumba, lakini Jumbe ndiye mwanaume aliyeweka historia tofauti ya maisha yangu.”
Wema akiwa na Jumbe.
MARA YA KWANZA KUSIMAMA MAHAKAMANI
Mwandishi: Historia ipi hiyo?
Wema: Nikiwa na Jumbe, pia nilikuwa na mgogoro na Kanumba na katika mgogoro huo, siku moja nilivunja kioo cha gari lake nikapelekwa Kituo cha Polisi Magomeni na baadaye Mahakama ya Wilaya Kinondoni.

Ingawa baadaye tulitakiwa kumaliza ishu nje ya mahakama, ikawa hivyo.“Mtuhumiwa mwenzangu alikuwa ni mdogo wake Jumbe ambaye kwa wakati huo naweza kusema alikuwa wifi yangu niliyependana naye sana, Asha Jumbe.
“Kusema ule ukweli ilikuwa mara yangu ya kwanza mimi Wema kusimama kizimbani. Ni kipindi ambacho nilimkera sana mama yangu.”Mwandishi: Nakumbuka ukiwa na Jumbe alitangaza kufunga ndoa na wewe, ilikuwa siriasi au danganya toto?
Wema: Tulikuwa siriasi na kama unakumbuka Jumbe alinivisha hadi pete ya uchumba na nasikia tulipoachana alikuwa akinitafuta ili nimrejeshee pete yake.“Unajua Jumbe ni mwanaume niliyekuwa nikipika na kupakua nyumbani kwake Tabata, tofauti na Chaz Baba.
Kuna waandishi wa Global Publishers, Ndauka (Oscar) na Luqman (Maloto), walishafika Tabata wakatukuta tulivyokuwa tunaishi kwa kupendana.
“Japokuwa ilikuwa vigumu kufunga ndoa na Jumbe kwa sababu mama hakumpenda kabisa, lakini sisi wenyewe tulikuwa tayari kwa hilo ndiyo maana nilikubali kuvaa pete yake.”
VIJEMBE VYA JUMBE NA MAMA WEMA
Mwandishi: Nakumbuka kuna wakati Jumbe alitupiana maneno na mama Wema, we ulikuwa unachukuliaje?
Wema: Unajua mama kama mama, alisimamia nafasi yake, Jumbe naye alisimamia kama mpenzi, naye alisimamia nafasi yake.

Mwandishi: Sasa mlipotangaza ndoa, mlifanya mchakato wote wa mambo ya uchumba, kama vile barua ya posa? Wema: Hapana. Kazi inakuwa pale mzazi mmoja anapokuwa hayupo tayari. Wakati mwingine ni vizuri kuamua tu, wanaokataa iko siku watakubali.
KWA NINI WALIMWAGANA NA JUMBE?
Mwandishi: Ni kwa nini mlimwagana na Jumbe?
Wema: “Ilitokea tu siku za mimi na yeye kuwa ‘separeti’ zilifika ikawa hivyo. Sidhani kama nataka kujua au kufafanua nini kilitokea lakini hatukuwa vizuri na tulitoleana maneno machafu kwenye media.

Uchunguzi wa gazeti hili wa hivi karibuni ulibaini kwamba, Jumbe ana mke, anaitwa Jack. Awali Jack aliwahi kuwa karibu na Wema kama mashoga na Jumbe alimnasa akitafsiriwa kuwa alifanya hivyo ili kumuumiza Wema baada ya kumwagana naye.
AENDA MAREKANI AKIWA WA CHAZ BABA, ARUDI AKIWA WA DIAMOND
Mwandishi: Nakumbuka ulipoondoka nchini kwenda Marekani mwaka 2010 ulikuwa na mpenzi Chaz Baba, lakini uliporejea ikasikika kwamba upo na Diamond, nini kilitokea Wema?
Mwandishi: Nakumbuka ulipoondoka nchini kwenda Marekani mwaka 2010 ulikuwa na mpenzi Chaz Baba, lakini uliporejea ikasikika kwamba upo na Diamond, nini kilitokea Wema?
Wema: (kicheko) yeah! Ni kweli kabisa, baada ya kuachana na Jumbe mwaka 2010 kama nilivyosema ndiyo nilianzana na Chaz Baba, nilimpenda, alinipenda.
Na yeye ilikuwa tuoane, lakini nimeshasema nikiwa Marekani nilikuwa nasikia leo Chaz alikuwa na huyu, kesho alikuwa na yule, nikamwambia mimi na yeye basi.
Mwandishi: Kwa Chaz Baba mama yako alimkubali awe mumeo?
Mwandishi: Kwa Chaz Baba mama yako alimkubali awe mumeo?