IRENE PAUL ~ SICHAGUI WALA SIBAGUI KWENYE MAPENZI

No Comments

Mtoto mzuri kwenye kilinge cha Bongo Movies, Irene Paul amefunguka kuwa kwenye suala la uhusiano, hana kipingamizi sana kwani anachoangalia ni mtu anayempenda haijalishi dini wala kabila.

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni jijini Dar, Irene alisema licha yakuwa bado hajamuanika mpenzi wake lakini suala la dini, kabila kwake siyo ishu ya msingi zaidi anaangalia mapenzi ya dhati.

“Naangalia tu, mtu anayenipenda ananipenda kweli au anaigiza? Nikigundua ananipenda kweli, nampenda pia. Hata aweje huyo ndiye atakayekuwa wangu wa maisha,” alisema Irene.
@ GPL
back to top