



TIMU ya Barcelona imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Manchester City kwenye mpambano wa Hatua ya 16 Bora ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa Uwanja wa Nou Camp nchini Hispania na kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo.
Kwa matokeo hayo, Man City wameondolewa kwenye michuano hiyo kwa kufungwa jumla ya mabao 4-1. Nayo timu ya PSG ya Ufaransa ilifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen. Leverkusen wameondolewa baada ya kufungwa jumla ya mabao 6-1.