

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Amanda alisema, watu wengi wanadhani alivyoachana na Hamisi, hawaivi tena kitu ambacho siyo kweli kwani wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali.
“Sina ubaya na Hamis na wala hajawahi kunitendea vibaya kwa hiyo hata kama nitapata tatizo wakati wowote akipata taarifa ndiyo wa kwanza kuja, so bado tunapendana ila hatuwezi kurudiana tena,” alisema Amanda.