Gari lililobeba mwili wa marehemu George Tyson likiingia ndani ya Viwanja vya Leaders Club tayari kwa shughuli nzima ya kuuaga mwili wa marehemu Tyson.
Ndugu wa marehemu Tyson wakiongoza waombolezaji pamoja na watu waliobeba jeneza kwenda katika sehemu maalum iliyoandaliwa.
Mike Sangu pamoja na Bakari Makuka wakiwa wamebeba jeneza hilo pamoja na wanakamati wengine.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akiaga mwili wa marehemu George Otieno 'Tyson' katika Viwanja vya Leaders, Dar.
Meneja wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho akitoa salamu zake za mwisho kwa mwili wa marehemu.