MMOJA wa wasanii wakongwe katika muziki wa kizazi kipya Tanzania ni Hamis Mwinjuma anayefahamika zaidi kwa mashabiki kama MwanaFA.
Tokea aliposikika kwa mara ya kwanza mwaka 2002, alipotoa kibao chake cha Ingekuwa vipi, amebakia kuwa juu, licha ya ushindani mkubwa katika Bongo Fleva.
Kwa kutambua mchango wake katika sanaa, gazeti hili lilifanya naye mahojiano na kuzungumzia masuala mbalimbali.
Kwa kutambua mchango wake katika sanaa, gazeti hili lilifanya naye mahojiano na kuzungumzia masuala mbalimbali.
Swali: Kuna tofauti gani kati ya Mwana
FA wa mwaka 2002 na huyu wa 2014?
FA wa mwaka 2002 na huyu wa 2014?
FA: Kuna tofauti kubwa, yule wa mwaka 2002 alipofanya shoo yake ya kwanza alilipwa shilingi 50,000 kama msanii katika shoo iliyotayarishwa na Jimmy Kabwe, lakini huyu wa sasa aliweza kuandaa shoo yake (The Finest) ambayo kiingilio kilikuwa shilingi 50,000 kwa mtu mmoja, nadhani hii ni historia katika muziki wa Hip Hop.
Swali: Kwa uzoefu wako, nini hasa tatizo linalowakabili wasanii wa Tanzania, hasa kimaslahi?
FA: Tatizo ni system (mfumo), tunalinganishwa na wasanii wa nje bila kujua kitu ambacho wenzetu wamefanya hadi kuwa pale walipo. Muziki wetu tunauendesha kienyeji na kudhani tutaweza kuwafikia over the night.
Swali: Nini kifanyike?
FA: Kuna vitu vingi. Kiukweli wasanii wanahitaji kuwa na Record Lebo, upo mchanganyiko mkubwa sana wa watu kufanya kazi ambazo siyo zao. Kama kitu hiki kinakuwepo, maana yake ni kwamba kinamsimamia msanii katika shughuli zake zote, lakini mwisho wa siku kila mtu anapata anachostahili.
Kuna kitu kinaitwa VAC (Value Adding Chain). Hii ni kwa ajili ya kumuongezea thamani msanii. Kwa mfano ukiwa peke yako labda thamani ya shoo yako moja ni shilingi tano, anakuja mtu anakutengeneza hadi unafikia thamani ya shilingi ishirini.
Anakuambia kwa kuwa amekuongezea thamani, basi yeye atachukua shilingi nane na wewe ubaki na 12.
Lakini sisi wasanii, huenda kwa kutojua, ikiwa hivyo tutaona tunaibiwa, bila kufikiri kuwa thamani yetu imepandishwa kwa kiasi gani.
Lakini sisi wasanii, huenda kwa kutojua, ikiwa hivyo tutaona tunaibiwa, bila kufikiri kuwa thamani yetu imepandishwa kwa kiasi gani.
Kampuni kubwa zinatakiwa kuwekeza kwa wasanii, lakini hili haliwezi kutokea hadi sisi wenyewe tuwashawishi hawa jamaa kwamba tunaweza kufanya nao kazi.
Swali: Angalau masilahi kwa wasanii hivi sasa yamekuwa bora kuliko siku za nyuma, unafikiri ni kwa nini?
FA: Kujitambua, hivi sasa kidogo kuna uelewa kuliko zamani. Angalia kwa mfano shoo zote kubwa ambazo wasanii wa nje hualikwa kwa kulipwa fedha nyingi, wabongo wanawaburuza vibaya. Ni P Square wa Nigeria pekee ambao wakija wanafunika, lakini wengine wote tunawakalisha hivyo inatosha kudai malipo mazuri zaidi.
Swali: Kwa miaka 12 uliyoitumia kwenye muziki, unadhani umefikia malengo?
FA: Hapana, ila nimevuka zaidi ya nusu ya malengo niliyojiwekea na kwa jinsi mambo yanavyokwenda, Inshaalah, matumaini yapo.
Swali: Muziki umekupatia kitu gani cha kujivunia kwa kipindi hicho chote?
Swali: Muziki umekupatia kitu gani cha kujivunia kwa kipindi hicho chote?
FA: Connections. Siwezi kusema kama watoto wadogo wanavyosema kuwa nina hiki au kile, kwangu mimi muziki umeniwezesha kupata connections nzuri sana. Katika watu muhimu wa nchi hii, nusu yao ninawafahamu. Kutokana na hilo, nina uhakika katika hao nusu, wanafahamiana pia na nusu iliyobaki, kwa maana hiyo niko katika chain ya watu muhimu, hilo ni jambo kubwa sana kwangu.
Swali: Muziki wetu umeshindwa kupenya katika soko la kimataifa, unafikiri kwa nini?
FA: Lugha. Kuna idadi ndogo sana ya watanzania wanaoweza kuzungumza lugha ya dunia (Kiingereza) kwa ufasaha na ili ulifikie soko hilo, ni lazima uzungumze lugha ambayo inakuelewa. Na kiukweli, sisi katika muziki hatutafuti kusikika sana nje, muhimu ni maisha, je unapata maisha kwa muziki?
FA: Lugha. Kuna idadi ndogo sana ya watanzania wanaoweza kuzungumza lugha ya dunia (Kiingereza) kwa ufasaha na ili ulifikie soko hilo, ni lazima uzungumze lugha ambayo inakuelewa. Na kiukweli, sisi katika muziki hatutafuti kusikika sana nje, muhimu ni maisha, je unapata maisha kwa muziki?
Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kati zenye watu zaidi ya milioni 160. Kama kunakuwa na mipango, hawa wanatosha kabisa kuwafanya wasanii wa nchi hizi kuishi vizuri kimuziki. Kama watu asilimia tano tu ya hawa wananunua kazi yako, wewe ni mtu tofauti kabisa.
Tulienda Afrika Kusini mwaka jana na kufika nyumbani kwa msanii mmoja anaitwa Oskido, aisee, ni balaa. Jamaa ana bonge la jumba na ana gereji ndani, full magari ya maana, tena brand new.
Lakini huyo jamaa nadhani hata wewe humfahamu, hasikiki nje ya Sauzi, lakini kwa sababu wenzetu wana mfumo mzuri wa uuzwaji wa kazi za wasanii, soko lao la ndani linajitosheleza sana.
Swali: Vijana wengi wanajitokeza na kufanya vizuri katika Bongo Fleva kiasi cha kuwatisha wakongwe, unawazungumziaje?
FA: Huwezi kuwazuia na wala hawana tishio lolote kwa sababu soko la muziki ni pana sana, tatizo ni moja tu kwamba wasanii tunataka kugombea kula tukiwa tumekaa sehemu moja, wakati inawezekana kabisa tukaweka chakula mezani na kila mtu akala kutokea upande aliokaa.
Msanii kama Diamond anafanya vizuri hivi sasa, lakini yeye hawezi kuzuia mtu mwingine kupata riziki kupitia muziki, redio haziwezi kupiga nyimbo zake kuanzia asubuhi hadi jioni na wala hawezi kupiga shoo zote peke yake. Kwangu mimi sioni kama wasanii wanaoibuka wanahatarisha chochote zaidi ya kuzidisha ushindani kitu ambacho ni kizuri.
Swali: Vipi kuhusu kuoa, bado upo upo sana?
FA: Yeah, bado kidogo ila nina mtoto ambaye nimezaa na mpenzi wangu wa muda mrefu sana. Ninaye tokea mwaka 2004, ingawa anaishi kwa mama yake lakini nina kazi ya kwenda kumuona kila siku, hapa nikimaliza kuongea na wewe ninaenda. Mwanangu anaitwa Malika.
Swali: Nini mipango yako ya baadaye kuhusu muziki?
FA: Nimewekeza muda wangu mwingi sana katika muziki, nina malengo nayo ya mbali mno. Niko katika mazungumzo na kampuni moja kubwa ili iweze kunidhamini katika mradi mmoja hivi ambao naamini uko vizuri. Ninaufikiria muziki kama biashara, siyo kwa ajili ya kupata sifa.
Swali: Umeshafanya kolabo na wasanii gani wa nje?
FA: Nimewahi kufanya na msanii mmoja wa Nigeria anaitwa Ash Hamman ngoma inaitwa Give it to me, pia nimefanya na Wyre, Prezo, Bamboo na Abbas Kubaff wote wa Kenya, Chameleone na Michael Ross wa Uganda na HHP wa Afrika Kusini.
Swali: Nje ya muziki, unapenda nini zaidi?
FA: Kwanza, muziki kwangu ndiyo kila kitu, vitu vingine vyote vinakuja baada ya muziki, lakini mimi ni shabiki mkubwa sana wa soka, hapa nyumbani ni Simba na Coastal Union, nje ni Manchester United damu, lakini pia napenda Boxing na Basketball.
Swali: Unafuatilia siasa?
FA: Sana, usipojua siasa maana yake hujui nchi yako inavyokwenda, ninafuatilia sana siasa.
FA: Sana, usipojua siasa maana yake hujui nchi yako inavyokwenda, ninafuatilia sana siasa.
Swali: Unazungumziaje juu ya kilichotokea katika Bunge la Katiba kwa Ukawa kutoka mjengoni?
FA: Kila upande una hoja, kitu cha msingi ni watu kujadiliana kama watu wazima, lakini bahati mbaya hatuoni kama wanafanya hivyo. Kwangu mimi, nafikiri muundo wa muungano wa serikali mbili ni mzuri zaidi, uko real zaidi kuliko serikali tatu. Kama msimamo wa Ukawa utaendelea hivi, sidhani kama katiba mpya itapatikana.
Swali: Mwisho, unaweza kuzungumzia lolote juu ya ugomvi wako na Lady Jaydee?
FA: Hapana. Yale yalishapita, maisha yanaendelea.
Swali: Mwisho, unaweza kuzungumzia lolote juu ya ugomvi wako na Lady Jaydee?
FA: Hapana. Yale yalishapita, maisha yanaendelea.