JEMBE limeondoka! Ndiyo... ilikuwa unaweza kumfananisha Adamu Kuambiana na jembe kwenye kilimo! Jembe likikosekana, maana yake mkulima hawezi kuendelea kulima na mwisho wake ni kukosa mazao.Ni siku ya tano sasa tangu Adam atutoke. Kwenye tasnia ya sinema ni pigo kubwa. Marehemu Kuambiana alifariki ghalfa, Jumamosi ya Mei 17, mwaka huu akiwa njiani akipelekwa hospitalini.
Msanii huyo alikutwa ameanguka chooni asubuhi hiyo, muda ambao alifuatwa na wenzake kwa ajili ya kuelekea ‘location’ kuendelea kurekodi sinema mpya ya Jojo. Hiyo ilikuwa sinema ya kwanza kuandaliwa na yeye mwenyewe baada ya kushiriki filamu nyingi za kushirikishwa.
Yeye na wenzake walikuwa wameweka kambi Silvarado Lodge, iliyopo Sinza ya Kwaremmy, Dar. Alikutwa amezidiwa na alikuwa akilalamikia maumivu makali ya tumbo. Madaktari wa Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge ndiyo waliothibitisha kifo chake.
Bila unafiki, marehemu Kuambiana aliishi maisha yake halisi. Hakuishi maisha ya kuigiza, kujifanya matawi ya juu na maringo. Alikuwa mcheshi na ‘serious’ sana kwenye kazi. Mara kadhaa alitofautiana na wasanii wenzake location akiwa anaongoza sinema.
Hakupenda mizaha kwenye kazi. Kuambiana alikuwa mtu wa utani sana lakini akishasema: Action... anataka kuona msanii akiigiza vile alivyomwelekeza. Ndivyo Kuambiana alivyokuwa.
UBUNIFU
Kuambiana alikuwa mbunifu sana. Angalia sinema zake nyingi alizotunga, zina ubora mkubwa. Msanii Jacob Steven ‘JB’ ndiye ambaye anaweza kuthibitisha zaidi ninachokisema maana amefanya naye kazi nyingi.

Sinema nyingi za JB ni kiwango. Zipo alizotunga marehemu Kuambiana, nyingine ameigiza na kuongoza au kimojawapo.
Nitakukumbusha. Sinema ya Regina ndiyo iliyomwonyesha kuwa habahatishi, hapo ilikuwa baada ya kung’aa na Fake Pastors ikitanguliwa na Sauti ya Manka ambayo haikufahamika sana. Kwenye Regina Kuambiana aliandika stori, kuigiza kama mhusika mkuu msaidizi na muongozaji.
MWONGOZAJI MKALI
Hakuna shaka yoyote kwenye kuongoza alikuwa na uwezo wa aina yake. Kwa wapenzi wa sinema watakubaliana nami.
Ukiachana na Regina, Dj Ben iliyomshirikisha JB, Wema Sepetu na wengineo pia kuna sinema kama Hukumu ya Ndoa Yangu, Born Again, Dereva Taksi, Vita Baridi, Lerato, 14 Days, My Fiance, Danija, Basilisa, Chaguo Langu na nyinginezo.

Ninaposema anaweza kuongoza ninamaanisha, maana kuna wakati nilishuhudia akifanya kazi. Enzi za uhai wake, nakumbuka msanii mkongwe, Hashim Kambi ‘Ramsey’ aliwahi kunipigia simu na kuniambia kuna nafasi ya kuigiza kwenye sinema ya Born Again iliyotayarishwa na JB na akaniomba nishiriki.
Nilikubali. Nilikwenda hadi ‘location’ nikamkuta Kuambiana kazini. Katika sinema hiyo, nilicheza ‘scene’ tatu, moja ikinikutanisha na JB, nyingne na Ramsey na ya mwisho na wazee wengine ambao siwakumbuki majina.
Kiukweli Kuambiana alikuwa na kipaji cha kipekee.
Hadi mauti yanamkuta, alicheza zaidi ya sinema 40, kuongoza zaidi ya filamu 30 na kuandika hadithi za sinema zaidi ya 25. Achana na zile alizoweka tafsiri ya maneno (sub titles). Ama kwa hakika jembe limeondoka!

ALIISHI KIRAFIKI ZAIDI
Mapenzi mema na wasanii wenzake ndiyo msingi aliojijengea. Tangu taarifa za kifo chake zilipoanza kuenea, wasanii wengi walionekana wakilia wengine hadi kuzimia.
Mapenzi mema na wasanii wenzake ndiyo msingi aliojijengea. Tangu taarifa za kifo chake zilipoanza kuenea, wasanii wengi walionekana wakilia wengine hadi kuzimia.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengele ‘Nyerere’, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ wanaweza kuwa wawikilishi wa wengine wengi waliozidiwa kwa kububujikwa na machozi.
Hawa walionekana katika Hospitali ya Mama Ngoma, mapema Jumamosi baada ya taarifa za kifo chake kuzagaa.
Jumatatu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wasanii walionekana kuishiwa nguvu wakati mwili wake ukitolewa kwa safari ya kupelekwa nyumbani kwake, Bunju. Simanzi iliibuka zaidi katika Viwanja vya Leaders Club, jana wakati akiagwa kwenye misa maalum iliyofanyika viwanjani hapo na baadaye kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika Makaburi ya Kinondoni.
Huo ukawa mwisho wake – mwisho wa enzi. Pumzika kwa amani Jembe. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake