MKALI wa kuvurugwa, Snura Mushi ‘Snura’ ameweka plain kuwa anaweza kuuweka pembeni kwa muda muziki wa mduara na kuimba muziki wa taarabu kutokana na maoni ya mashabiki.
Akifunguka katika mahojiano maalum na Global TV Online, Snura alipoulizwa kuwa atafanya muziki wa mduara hadi lini ndipo alipobainisha kuwa anaweza kubadilika na tayari ana wimbo wa taarabu ameshaufanya.