KUMBUKUMBU YA KANUMBA YAMJENGA WOLPER KIIMANI

No Comments
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amesema kila anapofikiria kifo cha aliyekuwa gwiji wa filamu  chini, marehemu Steven Kanumba anajikuta akizidisha ibada na kumtukuza Mungu wake.
Wolper akielekea kwenye kaburi la Kanumba.
Akizungumza  Wolper alisema, katika hali ya kawaida kwa maisha wanayoishi mastaa ya kupenda kujiachia, wengi wamekuwa wakijisahau kuwa dunia ni mapito na kuona kama ni makazi ya milele dhana ambayo ni potofu.
“Siyo siri kila ninapofi kiria kifo cha Kanumba imani yangu inajiongeza, nazidisha kumtumikia vyema Mungu wangu kwani  uala la kifo halina taarifa, linaweza kukukuta muda wowote, nani alijua kama Kanumba angetutoka  kipindi kile hatimaye miaka miwili sasa ?”alihoji Wolper.
back to top