Uhali gani mpenzi msomaji wa safu hii. Ni matumaini yangu umzima kabisa na uko tayari kusoma muendelezo wa makala haya ambayo niliianza wiki iliyopita.
Maudhui hasa ya makala haya ni kuwatahadharisha baadhi ya watu ambao wanahusudu mapenzi kuliko kitu kingine utadhani wana pepo la ngono.
Sikatai, kufanya mapenzi ni kitu muhimu sana hasa kwa watu walioingia kwenye ndoa. Kwa kifupi ni haki ya kila mmoja kuridhishwa na mwenza wake pale anapojisikia lakini wakati mwingine tuwe watu wa kuzikontroo hisia zetu.
FARAGHA ISIKERE
Tusiwakere wenza wetu kwa kila mara kuhitaji kukutana faragha kwa kuwa, kama nilivyosema wiki iliyopita, kila jambo likipita kiwango ni tatizo (every thing too much is harmful) hivyo tujiwekee mfumo mzuri wa kupeana raha bila karaha.
Tusiwakere wenza wetu kwa kila mara kuhitaji kukutana faragha kwa kuwa, kama nilivyosema wiki iliyopita, kila jambo likipita kiwango ni tatizo (every thing too much is harmful) hivyo tujiwekee mfumo mzuri wa kupeana raha bila karaha.
Katika hili naomba nishauri yafuatayo; Kwanza tujitahidi kujitoa kwenye kundi la watu wenye pepo wa ngono. Tukiwa kwenye kundi hili, si kwa mwanaume tu hata kwa wanawake, ni lazima tutakuwa watu wa kuwaza ngono kila wakati.
Tushughulishe akili zetu kwa kufanya kazi na kuwaza mambo ya kimaendeleo.
Haya mambo unaweza kuyachukulia poa lakini kumbuka wapo walioachwa kwa kuendekeza mapenzi na wapo ambao wanachengwa na wapenzi wao kwa kuwa wasumbufu katika hili.
Haya mambo unaweza kuyachukulia poa lakini kumbuka wapo walioachwa kwa kuendekeza mapenzi na wapo ambao wanachengwa na wapenzi wao kwa kuwa wasumbufu katika hili.
Kila wakati…kila saa…kila wakikutana hakuna kingine zaidi ya mambo hayo, yanachosha jamani. Wakati mwingine mwenza wako anapokuwa na wewe anataka mzungumzie tu maisha sasa kama wewe utaanza stori za ngono, ni wazi utamchefua.
Pili ni kwamba, mapenzi ni kitu muhimu kwa wawili waliotokea kupendana na hili linatakiwa kufanyika kikamilifu. Unapokuwa faragha na mwenzao wako, onesha utundu na ubunifu wako wote
. Mfanye afurahi na akuone wewe ni wa kipekee. Kamwe usimpe kiduchu kwani kufanya hivyo ni kumfanya afikiri kwenda kwingine ambako anaweza kupewa akatosheka.
Tatu, tusifikie hatua ya kuwekeana ratiba katika hili. Wapo ambao wamekuwa wakinilalamikia kwamba, wake/waume zao hasa wale wanaofanya kazi wamekuwa wagumu sana kwenye suala la ‘kupeana mambo’, kisingizio kikiwa ni kuchoka kutokana na majukumu ya siku nzima.
Matokeo yake wanandoa hawa wanawawekea ratiba wenza wao kwamba watakuwa wakikutana siku za wikiendi tu, siku nyingine kila mmoja ageukie kwake.
Hapo ndipo baadhi ya wanandoa wanapojikuta wanakaribisha usaliti kwenye ndoa zao bila kujua. Hivi unapomuwekea mumeo au mkeo ratiba ya kukutana naye siku za wikiendi tu, siku nyingine akijisikie unataka aende wapi? Usimlazimishe mwenzako akutafutie msaidizi.
Anajisikia, wewe hujisikii, ufanyeje? Hili mbona linazungumzika? Kikubwa ni wewe kuwa muwazi kwa mwenza wako. Mwambie kwa lugha ya upole kwamba unaumwa au umechoka hivyo awe mvumilivu. Usitumie lugha ya ukali.
Lakini wakati mwingine kama unaona kuna njia nyingine unaweza kuitumia kumfanya afurahi, fanya hivyo kuliko kumwambia…’mimi sijisikii bwana’.
Kwa wale wenzangu na mimi ambao ni watundu na wabunifu kamwe hawawezi hata siku moja kuwaambia wenza wao kuwa wamechoka au hawajisikia, watatumia utundu wao kuwafanya wale waliotokeo kuwapenda wafurahi kwa kutumia mbinu wanazozijua wao.
Wewe huzijui mbinu hizo? Siwezi kuzianika kupitia ukurasa huu kwani ni mambo ya kikubwa yanayotakiwa kusomwa na watu wazima tu ila usikonde, waweza kuwasiliana nami kwa namba hizo hapo juu na nitakupa elimu ambayo naamini itakufaa kwenye ndoa yako.
Ninachotaka kusema Leo ni kwamba, mapenzi yanachukua nafasi kubwa sana kwenye maisha yetu lakini tuwe makini yasituharibie maisha yetu.
Wapo watu wanakera sana, unakuta mwanaume anafanya kazi lakini mchana lazima arudi nyumbani ‘kula chakula cha mchana’. Akirudi tena anataka ‘chakula cha jioni’. Usiku ndiyo anakula hadi anavimbiwa, hii siyo sawa!