
TAMASHA la Usiku wa Matumaini, Dar (Dar Night of Hope 2014) lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar lilikuwa ni full msisimko kutokana na matukio mbalimbali yaliyofanyika.
Staa kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Makamu wa Rais Mh. Mohamed Gharib Bilali akisalimiana Makamu wa rais Mh.Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na Miongoni mwa matukio yaliyosisimua kwenye tamasha hilo ni pale mechi za mpira wa miguu zilipokuwa zikichukua nafasi.
Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
BONGO MOVIES VS BONGO FLEVAWakati mechi hiyo ilipokuwa ikikaribia kuanza, umati ulilipuka kwa shangwe baada ya kumuona Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba alipokuwa alipoonekana akipasha misuli na wenzake.
Kama hiyo haitoshi haitoshi, shangwe zaidi liliongezeka baada ya Kiba kufunga bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya Bongo Fleva waibuke kidedea kwa mara nyingine hivi kumfanya kuwa nyota kwenye tamasha hilo.

Licha ya kufungwa, mashabiki wa Bongo Movies ndiyo walionesha kushangilia zaidi ya mashabiki wa Bongo Fleva ambao ndiyo walikuwa washindi.

Wakati wa mechi ya wabunge, vituko ndiyo ilikuwa balaa. Kuna wakati baadhi ya waheshimiwa wabunge walikuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kusogea lakini mwisho wa siku ilikuwa ni burudani kwani waliweza kubadilishana, wengine wakachukua nafasi. Hadi mtanange unamalizika, wabunge wa Yanga waliibuka kidededea kwa ushindi wa mabao 3 kwa 2.
Tamasha la Usiku wa Matumaini mwaka huu lilikuwa noma sana!