BELA, KALAMA NDOA YANUKIA

No Comments
Staa wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bela’.

STAA wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bela’ na mpenzi wake wa kitambo, Karama Omari ‘Luten’ wanatarajia kufunga ndoa Novemba, mwaka huu.


Akizungumza na mwanahabari wetu, Isabela ambaye anatamba na wimbo wa Taratibu alisema ana furaha isiyo na kifani kwani kwa mara ya kwanza tangu aanze uhusiano wa kimapenzi na Karama amemtamkia suala la ndoa.Msanii wa Bongo Fleva Karama Omari ‘Luten’ .
“Yaani nina furaha sana kwani Karama hakuwahi kunitamkia kwamba atanioa lakini hivi karibuni ametamka tena mbele za watu naamini ndoa yetu itakuwa ya baraka kwani mama Rolaa amejitolea kutufanyia sherehe ambapo ameahidi kutoa milioni tano, bado marafiki zake,” alisema Bela.
back to top