KUPENDA ni haki ya kila binadamu mwenye ukamilifu. Hata hivyo kulingana na mila na desturi zetu za Kiafrika wanaume ndiyo huanzisha uhusiano.Kwa utamaduni huo basi, mwanamke hukosa uhuru wa kufikisha hisia zake kwa chaguo lake huku mwanaume akiwa huru kutoa dukuduku lake pale anapohisi kupenda.
Pamoja na kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia yanamfanya mwanamke wa sasa awe na haki sawa na mwanaume, bado kumekuwa na ugumu kwa mwanamke kumwambia mwanaume kuwa anampenda na angependa kuwa mpenzi wake.
Mwanamke wa aina hiyo, huonekana muhuni, asiyejiheshimu. Lakini kuna jambo moja la msingi hapa kulijadili; ni pale mwanamke anapotongozwa na mwanaume asiye chaguo lake. Wakati mwingine inawezekana hata hajatongozwa, lakini dalili za mwanaume huyo zikamfanya aone wazi kwamba anamtaka ila yeye moyoni mwake akawa hana nafasi kabisa.
Hapa ndipo wanawake wengi wanapobaki njia panda. Kwa bahati mbaya sana, wapo ambao huamua kuingia kwenye uhusiano kwa majaribio, jambo ambalo ni hatari kwenye uhusiano.
Inapotokea hali hiyo baadhi ya wanawake wanashindwa kujua la kufanya na kufikiri labda kuwajibu majibu ya hovyo huweza kufikisha hisia zao na kuachwa kusumbuliwa.
Inapotokea hali hiyo baadhi ya wanawake wanashindwa kujua la kufanya na kufikiri labda kuwajibu majibu ya hovyo huweza kufikisha hisia zao na kuachwa kusumbuliwa.
Kama yupo mwanaume anayekusumbua mara kadhaa na wakati mwingine kuona kuwa ni kero kwako na hujui cha kufanya, usijali fungua ubongo ili uweze kuongeza kitu kipya.
Zipo njia za kumweleza mwanaume husika humuhitaji kistaarabu na yeye asijisikie vibaya na ukamuacha akiwa mwenye kukuheshimu.
Zipo njia za kumweleza mwanaume husika humuhitaji kistaarabu na yeye asijisikie vibaya na ukamuacha akiwa mwenye kukuheshimu.
MWANAMKE WA AINA GANI?
Kama upo kwenye ndoa yako, vipengele vifuatavyo hapa chini havitakuhusu kabisa, maana mwanaume anayemtongoza mke wa mtu, jibu lake ni muhuni.Hana staha na hafai kuthaminiwa na kupewa heshima ninayoizugumzia katika mada hii. Kwanza, mke wa mtu ana alama. Zipo nyingi na zinajulikana hasa kwa watu wanaomzunguka – wanamfahamu vizuri.
Ijulikane kwamba hata huyo mwanaume anayekutongoza, anakufahamu vizuri; ikiwa ni vinginevyo, huna sababu ya kujisumbua, huyo naye ni muhuni tu. Kama upo kwenye uchumba, una mwenzako anayejulikana au hata kama hajulikani, jibu lako ni jepesi tu, una mchumba!
Hutakuwa na sababu ya kutumia njia hii. Njia hii ni kwa wanawake ambao wako huru – wanasaka waume wa maisha yao, lakini kwa bahati mbaya, mwanaume aliyemtamkia mapenzi, si chaguo lake.
Nimetoa angalizo hilo kwa sababu, wanawake ambao tayari wako kwenye miliki za watu, si busara kuruhusu mawasiliano au mikutano na watu wasiyo wao tena kuzungumzia mapenzi.
Nimetoa angalizo hilo kwa sababu, wanawake ambao tayari wako kwenye miliki za watu, si busara kuruhusu mawasiliano au mikutano na watu wasiyo wao tena kuzungumzia mapenzi.
KUBALI KUMSIKILIZA
Hili linawashinda wengi, lakini waswahili walisema kubali wito, kataa neno. Kumsikiliza hakuna maana kuwa tayari umeshamkubalia. Kutana naye lakini jitahidi kukwepa sehemu zenye vificho au ambazo utakuwa na wasiwasi nazo. Kukubali kwako kutamfanya mwanaume huyo aone kuwa hujamdharau na unamheshimu.
MPE UHURU AJIELEZE
Onyesha kujali mazungumzo yake na kuwa makini kwa kila anachozungumza japokuwa tayari moyoni unatambua kuwa haupo tayari kuwa naye.Hakikisha anafahamu kuwa mawazo yako yapo pale, hii itamfanya awe huru kwako na kukueleza hisia zake kwa uwazi zaidi, inawezekana ukabadilisha mawazo na kuamua kuwa naye, hapo kazi ni kwako!