OTILIA SASA KUFUNGA NDOA BOMANI

No Comments
JAPOKUWA Mnenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Otilia Boniface alibadili dini na kuwa Muislamu baada ya kupata mchumba ambaye ni muumini wa dini hiyo, imebainika anatarajia kufunga ndoa ya bomani kutokana na ndugu zake kutoridhika na uamuzi wake wa awali.
Mnenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Otilia Boniface
Rafiki wa karibu wa Otilia aliyeomba hifadhi ya jina alisema kuwa, mnenguaji huyo aliyepata mchumba ambaye ni mume wa mtu lakini hivi karibuni mkewe alifariki dunia, ndugu zake wamekuja juu na kumtaka afunge ndoa ya bomani na siyo ya Kiislamu.
Akizungumzia hilo, Otilia alisema: “Ni kweli tutafunga ndoa ya bomani japokuwa tangu nilipoachana na mume wangu wa kwanza (Thabit) sikubadili dini tena, niko kwenye Uislamu na ndugu nao hawana hiyana kikubwa sasa wanamsubiri huyo mkwe wao.”
back to top