
Muigizaji mkongwe hapa nchini, Said Ngamba , maarufu kama mzee
Small ameiaga dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya taifa ya
muhimbili. Mzee Small alikua amelazwa akipatiwa matibabu.
Akithibitisha taarifa za kifo chake mtoto wake aitwaye Mahmoud
amesema baba yake amefariki majira ya saa nne usiku wakati akiwa
hospitalini hapo akiendelea kupatiwa matibabu.
Mipango inafanyika nyumbani kwake Tabata.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,Amen.