
Tingatinga la Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu [CDA], likibomoa moja ya nyumba zilizopo katika hifadhi ya Barabara inayotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni, ambapo zaidi ya nyumba 65 zilibomolewa katika eneo hilo la Mlamwa Kusini.

Wanawake wa mtaa wa Mlimwa wakimsaidia mwenzao aliyezirai baada ya tingatinga la CDA kufika kwa ajili ya kubomoa nyumba yake kupisha ujenzi wa barabara, zoezi hilo lilifanyika jana ambapo nyumba zaidi ya 65 zilibomolewa na kuacha familia zaidi ya 150 zikikosa makazi.

Mwenyekiti wa mtaa huo, Zubeda Haji akielekeza jambo wakati wa ubomoaji huo.

Wananchi wa Mlimwa waking'oa mabati muda mfupi kabla ya tingatinga la CDA kufika na kuibomoa nyumba hiyo ili kupisha hifadhi ya barabara.

Bibi huyu mkazi wa Mlimwa Kusini ambaye hakufahamika jina lake akiwa hajui la kufanya baada ya nyumba yake aliyokuwa akiishi iliyojengwa kwa mtindo wa tembe kubomolewa na kuachwa na vyombo vyake alivyoweka kwenye shamba la mahindi.



Wananchi wa Mlimwa Kusini wakiwa katika hekaheka ya kuhamisha mizigo yao na kukimbia nyumba zao baada ya kupata taarifa za ujio wa tingatinga la CDA kwa ajili ya kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.
PICHA NA JOHN BANDA WA: PAMOJA BLOG