WARAKA MZITO WA RAY C KWA LORD EYEZ

No Comments
Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ almaarufu Kiuno Bila Mfupa amemwandikia waraka mzito aliyewahi kuwa mwandani wake, Rapa Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ akimtaka kubadili ‘laifu staili’ yake.

Lord Eyez  katika pozi.
Ray C alimwandikia waraka huo Lord Eyez wa Nako 2 Nako Soldiers juzi ikiwa ni saa chache tangu aliposimamishwa kazi katika Kampuni ya Weusi baada ya kutuhumiwa kwa wizi wa kompyuta mpakato (laptop) jijini Arusha hivi karibuni.
Huku akitanguliza picha ya ‘Mnako’ huyo akisindikizwa na polisi, Ray C aliandika waraka huo kwenye ukurasa wake wa Instagram:
“Badilika babaa…nakuombea sana ujitambue na ubadili mwenendo wa maisha yako…wewe bado ni kijana mdogo sana na una kipaji cha kipekee…
“Kila mtu ana changamoto yake ya kimaisha …angalia wapi ulipokosea, litambue tatizo lako halafu kubali kwamba una tatizo then (halafu) rekebisha hilo tatizo…anza maisha mapya.
“Badilika…Majanga yote yanayokukuta ni ishara tosha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba unakoelekea siko.
“Kama una akili timamu basi utagundua hilo na utajirekebisha babaa.
“Nakuombea kila la kheri katika mabadiliko ya maisha yako…Karibu kwenye tiba ya Methadone… Methadone kiboko ya madawa (ya kulevya).”
Baada ya kutundika waraka huo, mashabiki wa Ray C walimpongeza kwa kutokuwa na kinyongo na Lord Eyez na zaidi kilichoonekana ni kwamba bado anampenda hivyo anamtakia mema.
Katika tuhuma inayomkabili Lord Eyez, anadaiwa kuvunja kioo cha gari la mwanamke mmoja jijini Arusha kisha kukwapua laptop hiyo iliyokuwa na ‘dokumenti’ muhimu hivyo anasubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Gazeti hili lilipowasiliana na Lord Eyez kwa njia ya simu hakupatikana na uongozi wa Weusi chini ya msemaji wake, Nikki wa Pili umesema kuwa kwa sasa hautamzungumzia rapa huyo hadi atakapomaliza tatizo lake.
Mwaka jana Lord Eyez alituhumiwa kwa wizi wa power window za gari la msanii Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’ ambapo alikamatwa na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Kinondoni, Dar huku Ray C akidai kuwa jamaa huyo ndiye aliyemwingiza kwenye unga akimtaka aachane na ‘hiyo kitu’.
back to top