Lazima tujifunze kuangalia mambo yenye umuhimu katika mapenzi. Wiki iliyopita nilieleza kuwa, kama mtu asipokuwa makini anaweza kujikuta anajiweka mbali na mafanikio kwa sababu ya matumizi makubwa kwenye mapenzi.
Marafiki, muungwana hujifunza kutokana na makosa, huu ni wakati wako wa kujifunza na kukubali makosa uliyoyafanya, kisha kuchukua hatua. Usikubali mapenzi yakusababishie hasara katika maisha yako, kataa kabisa kurudi nyuma kimaendeleo kwa sababu ya mapenzi. Bado unayo nafasi ya kubadilika!
UMEACHANA NA WANGAPI?
Kuachwa kunauma sana, wakati mwingine hata kuacha huwa kuna maumivu yake. Hapo inategemea mhusika alikuwa katika sababu gani za kufanya hivyo. Hakuna anayependa kuachwa, maana kuachwa ni fedheha. Mtu hulazimika kuacha kutokana na tabia chafu anazokuwanazo mpenzi wake.

Mtu anapoachwa na mpenzi wake moyo wake huumia sana na wakati mwingine huweza kwenda mbali zaidi akifikiria labda ana kasoro fulani katika mwili wake, hili ni tatizo. Wapo ambao hawana kawaida ya kudumu na mpenzi mmoja.
Kila siku anaanzisha uhusiano mpya. Wanaume wa aina hii hawajisikii vibaya kumtema mwanamke mara baada ya kushiriki naye tendo la ngono, hii siyo tabia nzuri.
Ni hatari kuachana na msichana ambaye umeshakutana naye kimwili tena akiwa hana kosa na moyo wako ukathibitisha hilo.
Ni hatari kuachana na msichana ambaye umeshakutana naye kimwili tena akiwa hana kosa na moyo wako ukathibitisha hilo.
Machozi ya mtu asiye na hatia ni laana kwako katika maisha yako ya uhusiano unaofuata! Kama ni kweli mpenzi wako amekukosea makosa makubwa yanayokubalika kuachana unaweza kufanya hivyo lakini kwa kumwambia wazi kwamba tabia yake fulani hutaiweza.
Kosa kubwa ambalo halivumiliki ni usaliti, ikiwa ni kweli umemfumania mpenzi wako zaidi ya mara moja na habadiliki tabia yake hiyo mbaya, huna haja ya kubembelezana naye zaidi ya kumuacha aendelee na mambo yake lakini siyo kakosa kadogo tu, kama mmepanga ahadi ya kukutana halafu hajatokea tayari unamwambia unamuacha, hapo utakuwa hujengi bali unabomoa!
Kumuacha mpenzi bila kuwa na kosa ni wazi kwamba wakati unaanzisha naye uhusiano hukuwa na mapenzi naye ya dhati. Kama ndivyo unatakiwa ufahamu kwamba utakuwa umempotezea muda mwenzako na madhara yanayoweza kutokea mbele yake ni mengi, kubwa zaidi ambalo unatakiwa kulifahamu ni kwamba kila chozi lake linapondoka ni laana kwako.
Unajua mapenzi yanaweza kukupa furaha lakini wakati huohuo yakakuhuzunisha moyo wako. Kuachwa ni kati ya madoa makubwa ambayo utakuwa umeyasababisha kwa kipindi chote ulichokuwa katika uhusiano.
Hata hivyo, doa hili lina pande mbili, lazima uangalie sababu za kuachwa na mpenzi wako; ni wewe ulikuwa na makosa au ni yeye? Hapa lazima uulize moyo wako na ujipe majibu yakinifu ambayo hayaelemei upande wowote.
Kubali makosa yako, kama kuna mahali ulikosea lakini wakati huohuo unatakiwa kutulia na kujiweka sawa kwa ajili ya kuanza upya katika uhusiano unaofuata.
Ikiwa kuna makosa ambayo ulimfanyia mpenzi ambaye alikasirika na kuamua kuachana na wewe basi badilika, kuwa mpya.
Ikiwa kuna makosa ambayo ulimfanyia mpenzi ambaye alikasirika na kuamua kuachana na wewe basi badilika, kuwa mpya.
Kuachwa ni kujiwekea historia mbaya ya mapenzi, unaweza ukapata mwenzi mpya lakini akichunguza na kugundua kwamba ulishaachika hilo linakuwa tatizo kubwa kwako na inawezekana kabisa jamaa akafikiria kuachana na wewe.
Sababu kubwa hapo ikiwa ni kuamini kwamba hauna tabia njema. Pingana na kuachwa katika maisha yako, ishi jinsi mwenzi wako anavyotaka.
Kama kuna makosa ni vyema mkaelezana kuliko kuchukua hatua ya kujibizana hadi mwisho wa siku inafikia hatua ya kuachwa...
Kama kuna makosa ni vyema mkaelezana kuliko kuchukua hatua ya kujibizana hadi mwisho wa siku inafikia hatua ya kuachwa...