Mpenzi msomaji, wiki iliyopita mwanadada Wema Isaac Sepetu aliishia pale alipokutana na aliyekuwa staa mkubwa wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba. ENDELEA
…
“Basi wakati tunatoka na dada, tukamwona tena Maya (mwigizaji Mayasa Mrisho), akaniita nimsogelee, nikamwambia nina haraka. Maya alichukua namba yangu ya simu ya mkononi lakini akaisevu kwenye simu ya Kanumba, akanibipu na mimi nikasevu Steven Kanumba, nikaondoka zangu.
“Kabla sijafika mbali simu yangu ikaiata, kuangalia hivi ni jina nililolisevu muda mfupinyuma, Steven Kanumba, nikapokea akajitambulisha nikamwambia namba yake nimeisevu, yakaishia hapo.
“Ilikuwa jioni ya siku hiyohiyo, Kanumba alinitumia meseji ya salamu, uko poa? Nikamjibu niko poa. Kuanzia siku hiyo tukawa tumejengeana tabia ya kutumiana meseji kwa karibu wiki moja.
“Ilikuwa jioni ya siku hiyohiyo, Kanumba alinitumia meseji ya salamu, uko poa? Nikamjibu niko poa. Kuanzia siku hiyo tukawa tumejengeana tabia ya kutumiana meseji kwa karibu wiki moja.
“Siku nyingine alikuwa akinitumia meseji kuniuliza nimekula nini? Kwa sababu ni mwanamke ninayejitambua nikabaini nini lengo lake.
“Kuna siku tena alianza kuniuliza kama nina boyfriend, nilimjibu ninaye ingawa sikuwa na boyfriend wakati huo, akanielekeza alipo ni hotelini panaitwa Lamada, nikaenda.
“Nilipofika tulikaa kwenye bustani, akaanza kuniambia ananipenda sana, nikamsisitizia kwamba mimi nina boyfriend, akaniambia nimfikirie.
“Nilipofika tulikaa kwenye bustani, akaanza kuniambia ananipenda sana, nikamsisitizia kwamba mimi nina boyfriend, akaniambia nimfikirie.
Nakumbuka tulivyokuwa tunaondoka tukakisi.
“Wakati naondoka akaniomba nirudi tena kumkisi, nikakataa, akaniomba sana, nikarudi na kumkisi, mapenzi yetu yakaanzia hapo.
“Wakati naondoka akaniomba nirudi tena kumkisi, nikakataa, akaniomba sana, nikarudi na kumkisi, mapenzi yetu yakaanzia hapo.
“Kanumba aliniomba niwe msanii tukiwa ndani ya mapenzi, si kwamba alinichukua kuigiza ndipo tukawa wapenzi kama watu wengine wanavyofikiria.
“Muvi yangu ya kwanza ilikuwa The Point of No Return, ya pili ni Red Valentine, tatu ni Family Tears, ikaja White Maria, kuanzia hapo nikawa nimeshajikita katika fani ya uigizaji.”
Amani: Hebu tuzungumzie uhusiano wako na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambao katika uhusiano wenu, wewe ndiye uliandikwa zaidi kwenye magazeti, unakumbuka mlikutana wapi?
Amani: Hebu tuzungumzie uhusiano wako na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambao katika uhusiano wenu, wewe ndiye uliandikwa zaidi kwenye magazeti, unakumbuka mlikutana wapi?
Wema: “Mimi na Nasibu (Diamond), tuliwahi kukutana mara moja tu Bilicanas (klabu iliyopo Posta, Dar) na hatukuwahi kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangaliana sana so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwa hiyo tukawa tumepeana migongo, nilikuwa na rafiki zangu wawili.
“Baadaye nikamuona, akaniona yeye alikuwa na rafiki yake, hatukusalimiana, hatukufanya chochote.
“Mimi nilichukua vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu, tumesimama hapo nje nikawa naambiwa ‘yule ndiye ameimba Wimbo wa Kamwambie’, kipindi hicho nilikuwa namuona wa ajabu sana ila tu ‘alijiseksisha’ kiasi fulani (kicheko kirefu).

“Kipindi hicho mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba (Charles Gabriel, mwanamuziki wa dansi kwa sasa ni Prezidaa wa Mashujaa Musica) so nakumbuka hiyo ndiyo ilikuwa the first and last day tumeonana.
“Mimi nikasafiri, nikaenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndiyo ilikuwa hot na Mbagala ndiyo kai-release (kuiachia). Dada zd yaani just from the songs.
“Mimi nikasafiri, nikaenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndiyo ilikuwa hot na Mbagala ndiyo kai-release (kuiachia). Dada zd yaani just from the songs.
“Dada yangu wa kwanza ana miaka 14 yupo Marekani na hajawahi kurudi Bongo tangu aondoke, kwa hiyo alikuwa anaona Bongo inafanya vizuri sasa hivi akaniuliza kama tuna urafiki na Diamond nikasema siyo sana, tunajuana tu.
”Akaniambia nimwambia aende Marekani kufanya shoo kwa sababu kila sherehe tuliyokuwa tunaenda lazima watapiga Kamwambie halafu kila mtu anaipenda.
“So watu wakaanza kuniambia like ‘hebu find contact naye huku kuna mapromota aje kufanya shoo na kipindi hicho Profesa Jay (mwanamuziki Joseph Haule) ndiyo alikuwa amekuja, nikamwambia basi sawa mimi nitamtafuta.
“Nikamwambia Dada Rehema Chalamila ‘Ray C’ anitafutie contact (mawasiliano) ya Diamond.
“So siku moja nikaona ana-plan (amepanga) kwenda kufanya shoo London, Uingereza.
“So siku moja nikaona ana-plan (amepanga) kwenda kufanya shoo London, Uingereza.
“Nikamtafuta mtandaoni nikam-text (kumtumia ujumbe), nikamwambia ‘hey mambo vp, mzima, upo London’ akaniambia ‘No mamie sipo London sijui ni nini’ nikamwabia Wema hapa, nipo Marekani halafu una fans (mashabiki) wengi sana, akaniambia basi sawa, acha nimalize ishu ya London halafu nitakuambia.
“Basi tukajenga tu mazoea tukawa tunachati nini, yaani ikawa yeye anaingia Facebook kuchati na mimi naingia kuchati naye, washkaji tu yaani.
“Akawa ananiambia ‘bado uko na Chaz na nini’, nikamwambia yeah nipo na Chaz.
“Akawa ananiambia ‘bado uko na Chaz na nini’, nikamwambia yeah nipo na Chaz.
Sasa ilikuwa ni kama mwezi wa tisa kama sikosei. Mimi wakati nipo Marekani nilikuwa naambiwa sana habari kuhusu Chaz, mara Chaz sijui yupo na mwanamke gani, hiyohiyo Facebook watu wananitumia mpaka picha nikimuuliza anakataa.
“Sasa mimi nakumbuka dada yangu alikuwa anampenda sana Chaz, so siku ya siku amekutana naye yupo sijui na mwanamke gani alipoaniambia nikasema, basi. So nikajikuta namuelezea matatizo Diamond. Siku niliyoamua kabisa mimi and Chaz basi, nikamwambia mimi siwezi. So tukawa tunawasiliana na Nasibu hivyo.
“Siku moja tukanuniana, alikuwa amealikwa Ikulu halafu nikawa nam-text hajibu, nikimpigia simu hapokei akaja akatoka akanipigia simu nikawa sijibu. Akanitumia meseji ‘baby I am sorry, we ndiye faraja yangu sijui ni nini…. I LOVE YOU.