MSANII wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka ameibuka na jipya ambapo leo amefanya kampeni ya kusafisha jiji aliyoipa jila la Ng’arisha Tanzania ambapo wadau mbalimbali wamejitokeza wakiwemo viongozi wa serikali na wasanii wenzake.
Kampeni hiyo imefanyika katika wilaya ya Ilala ambapo walianza kufagia kuanzia maeneo ya Lumumba mpaka Mnazi Mmoja.