NDOA YA CATHY YACHOKONELEWA

No Comments
MKONGWE Bongo Movies, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa kuna mwanamke ambaye anaichokonoa ndoa yake kwa nia ya kuivunja.

Sabrina Rupia ‘Cathy’.
Akizungumza na mwandishi wetu, Cathy alisema amechunguza na kugundua kuna mwanamke ambaye anatuma meseji kwa mumewe na kwake kwa lengo la kuwagombanisha.
“Anatumia kila njia kuisambaratisha ndoa yangu, anajisumbua, najua ni mwanamke sababu nimeshafanya uchunguzi wangu kwa kuipiga hiyo namba, ole wake nimdake, atanitambua,” alisema Cathy.
back to top